Tuesday, August 30, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA 36 WA SADC MJINI MBABANE SWAZILAND

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini ubao wa kumbukumbu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wenye majina ya viongozi waliohudhuria mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika Lozitha, Mbabane Swaziland.

WAZIRI MBARAWA AFUNGUA KOZI MPYA YA MAFUNZO YA WAKUFUNZI WA MARUBANI

Rubani Focus Mmbaga kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), akitoa maelezo ya namna ndege inavyoendeshwa kwa kutumia kifaa maalum cha mafunzo ya urubani (simulator) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani uliofanyika jijini Dar es salaam. 

Monday, August 29, 2016


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ameendelea kugoma kula kwa siku ya tatu mfululizo tangu alipokamatwa Oktoba 26 mwaka huu, nyumbani kwake mjini hapa, akidaiwa kutoa maneno ya uchochezi.
 Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku ya kwanza walipokutana wakati wa maandalizi ya kutengeneza kipindi hicho.
Mohammed Hammie na Happy Balisidya wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kufahamu watakuwa wakiendesha kipindi cha CHUKUA HATUA.
---
Chukua Hatua ni kipindi kipya cha radio kitakachowashirikisha vijana, wakizungumza na kujadili kwa pamoja masuala yanayowahusu hasa ya kujikwamua na maendeleo mkoani Dodoma na maeneo jirani.
Hiki ni kipindi ambacho kinatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za ajira kwa vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa vijana wa kike na kiume.
Lengo kuu la kipindi hiki ni kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira na changamoto wanazokutana nazo katika mihangaiko yao, kipindi kitapaza sauti za vijana ambazo hazikupata nafasi ya kusikika hapo kabla.
Si kipindi tu, bali pia ni jukwaa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi, mawazo, uzoefu na pia kujifunza kutoka kwa wengine, ni mahala pekee ambapo kijana atayaona matarajio na uzoefu kutoka fani na taaluma mbalimbali.
Kipindi pia kinatarajiwa kuimarisha ujuzi na kuelekeza upya akili za vijana kufanya kazi na kuchangamkia fursa za ajira kwa ujasiriamali, kujiajiri na kuukwepa umaskini uliokithiri miongoni mwao.
Kipindi kitaanza kuruka hewani siku ya Alhamisi ya tarehe 01/09/2016 kupitia kituo cha RASI FM RADIO inayopatika masafa ya 103.7 Dodoma.
Pia kipindi kitakuwa kinapatikana kupitia mtandao wa Youtube ukurasa wa CHUKUA HATUA, pia mijadala itakuwa inaendelea kupitia ukurasa wetu wa facebook ambao ni CHUKUA HATUA, Instagram ni KIJANA CHUKUA HATUA, na Twitter ni CHUKUA HATUA1
Kipindi hiki kimewezeshwa na mpango wa pamoja wa ajira kwa vijana wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kazi Duniani (ILO) kwa udhamini wa SIDA.

JPM NA LOWASSA WAMEONYESHA KUWA MAZUNGUMZO YATALETA MUAFAKA.

Waziri Mkuu wa zamani Mh.Edward Lowassa akisalimiana na Rais Dkt John Pombe Magufuli

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NCHINI SWAZILAND,KUMUWAKILISHA RAIS MKUTANO WA 36 WA SADC

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ardhi ya mji wa Mbabane nchini Swaziland tayari kuhudhuria mkutano wa 36 wa SADC wa Wakuu wa nchi  na Serikali ambao utafanyika tarehe 29 Agosti mjini hapo.

Friday, August 26, 2016

GODBLESS LEMA ATIWA MBARONI NA JESHI LA POLISI


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA)  amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake alfajiri  ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.

Na huko mkoani Kigoma Jeshi la Polisi liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI MKUTANO WA APRM- NAIROBI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika maungumzo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya (kulia), Rais wa Msumbiji,  Filipe Nyusi (wapili kulia) na Mwenyekiti  wa Umoja wa Afrika (AU), Madame Nkosazana Dlamini- Zuma kabla ya kuanza kwa Mkutano wa African Peer  Review Mechanism Forum (APRM) kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UHU2
UHU3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa African Peer  Review Mechanism Forum (APRM)kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016.
UHU4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakishiriki katika Mkutano wa African Peer  Review Mechanism Forum (APRM)kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, August 25, 2016

MAJALIWA: WAKURUGENZI WAHAMASISHENI WALIMU KUJIENDELEZA KIELIMU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na Maofisa Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa Elimu Kata na Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa shule za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma. 

MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI YAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba  miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi    katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi  vilivyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.

Wednesday, August 24, 2016

KESI YA TUNDU LISSU YAIHIRISHWA































Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi – Kisutu, Yohanne Yongolo ameihairisha kesi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu hadi Septemba 6 mwaka huu ili kutoa uamuzi wa maombi yaliyoombwa na upande wa mshtakiwa.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATEUA MKURUGENZI MKUU WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA





 Dkt. Modestus Francis Kipilimba-Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro, wakati walipokuwa eneo la tukio.

Tuesday, August 23, 2016

MAJALIWA AKIWASALIMU WANANCHI WA KIJIJI CHA MAJIMOTO WILAYANI MLELE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa kijiji cha Majimoto wialyani Mlele kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo, Agosti23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KIKAO CHA EDWARD LOWASSA CHAZUIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

 Kikao cha ndani cha Mh.Edward Lowassa na wanachama wa Chadema wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kimezuiwa kufanyika na Jeshi la Polisi .

MARUFUKU oparesheni UKUTA JIJINI DAR

 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha site Mirror zilizoibwa katika magari leo jijini Dar es Salaam.

Monday, August 22, 2016

RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MAENDELEO YA UJENZI WA KIWANDA CHA KUSINDIKA GESI ASILIA (LNG)

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Kampuni ya Mafuta ya Stat Oil ya Norway, Bw. Oystein Michelsen kabla ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.

CHANZO CHA KUVURUGIKA MKUTANO WA CUF HIKI HAPA

Mkutano mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ulioketi jana jijini Dar es Salaam ulivurugika pasipo malengo ya mkutano huo kufanikiwa.Mkutano huo ulilenga kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa ngazi za juu pamoja na kujadili barua ya kujiudhuru na ya kutengua kujiudhuru ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba.

LOWASSA, MBOWE NA KATIBU MKUU CHADEMA WAANZA MIKAKATI YA UKUTA


Siku moja baada ya Chadema kutangaza safu ya Ukuta, viongozi wa chama hicho wameanza kutawanyika mikoani kuanza kutoa elimu ya mpango huo. 

Wakati mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwa Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa alikuwa mkoani Mbeya na jana alishiriki ibada na kuanza vikao vya mkakati huo. 

Thursday, August 18, 2016

RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA ARUSHA FELIX NTIBENDA,AMTEUA MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA

 Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na Rais,kuapishwa  ijumaa Ikulu jijini Dar.

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO MFUMO WA HEWA NA NJIA YA MKOJO

Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula kwa kushirikiana na Profesa Saber M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri. 

BALOZI WA ISRAEL NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI MAKAMBA.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh. Yahel Vilan alimpomtembelea Waziri Makamba  Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam.

SERIKALI YAMPONGEZA MWANDISHI WA KAMUSI YA UKRISTO


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko (katikati), Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri wakiwa wameshikilia Kamusi hiyo mara baada ya Uzinduzi 17 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Tuesday, August 16, 2016

MAKONDA AYAOMBA MASHIRIKA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mbalimbali jijini Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la uchangiaji wa hiari wa madawati kwa shule za msingi linaoendelea jijini humo ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia yatakayozalisha wanafunzi bora wa shule za msingi.

KUNDI LA ORIGINAL COMEDY LAINGIA MATATANI KWA KUVAA SARE ZA POLISI KWENYE HARUSI YA MASANJA MKANDAMIZAJI

Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi. 

MBUNGE WA MKURANGA,MH. ULEGA AKABIDHI MADAWATI 537 HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA.

Mbunge Abdallah Ulega (katika alie simama) akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Msham Munde, mkuu wa wilaya hiyo Filberto Sanga, na mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke mara baada ya kukabidhi madawati 537 ya mbunge wilayani humo.

MPANGO MKUBWA UMEME NCHINI WAZINDULIWA, KAYA 500,000 KUPATA UMEME WA UHAKIKA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza huku akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa mpango wa TREEP katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird 

Saturday, August 13, 2016

KAMATI YA UONGOZI YA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA YAKUTANA


Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi wa Baraza hilo kilichokutana kujadili hali ya siasa Jijini Dar es Salaam.

PROFESA BAREGU AONGOZA KONGAMANO LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA) UKUMBI WA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mesigwa Baregu (kulia), akizungumza katika kongamano la Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha), ikiwa ni maadhimisho ya siku ya vijana duniani lililofanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtoa mada katika kongamano hilo, David Kafulila.

RAIS MAGUFULI APOKELEWA KWA SHANGWE KATIKA OFISI YA CCM LUMUMBA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia kuwasalimia wanaCCM waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam akitokea jijini Mwanza.

WAHANDISI WANAWAKE NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAMPENI YA KUSHAWISHI WATOTO WA KIKE KUSOMA SAYANSI NA HISABATI

 Makamu Rais ametoa kauli hiyo 12-Aug-16 wakati anafungua kongamano la maonyesho ya kitengo cha wahandisi wanawake cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Amesisitiza kuwa kampeni hiyo itasaidia kuelimisha wasichana,kuwaunganisha na kuwaendeleza watoto wa kike ili waweze kujitambua na kuithamini nafasi yao katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia fani za sayansi na teknolojia.

Thursday, August 11, 2016

Chadema waijadili barua ya Jaji Kaganda

Hiki ndicho walichokijibu viongozi wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, mara baada ya kupokea barua kutoka Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma iliyoeleza jinsi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mwanasheria Mkuu Tundu Lissu.

WARATIBU WA MIRADI YA MAENDELEO TEMEKE WATAKIWA KUCHORA RAMANI YA MAENEO YA MRADI- HASSAN

 Mhandisi kutoka kampuni ya Kyondonga ya nchini Korea, Lee akielezea mradi wa maendeleo wa uboreshaji wa miundo mbinu ambapo wameingia mkataba na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikishirikisha jumla ya kata 13.

GAZETI LA MSETO LAFUNGIWA KWA MIEZI 36


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifungia kwa miezi 36  gazeti la “MSETO”. Amri ya kulifungia  Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 242 lililotolewa tarehe 10 Agosti, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 Sura ya 229, kifungu 25(1).

MAHAKAMA KUU YATENGUA HUKUMU YA AWALI YA KUWAFUTIA SHTAKA LA UTAKATISHAJI FEDHA ALIYEKUWA KAMISHNA MKUU WA TRA NA WENZAKE


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Emmilius Mchauru wa kufuta shtaka la kutakatisha Dola Milioni 6 za Kimarekani baada ya kuona liliondolewa kinyume cha sheria!

Kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (pichani kati) Harry Kitilya na wenzake dhidi ya mashtaka manane ikiwamo la kutakatisha fedha na walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi Mwaka huu. 

NAIBU KATIBU MKUU PROFESA JAMES MDOE ATEMBELEA MNADA WA TANZANITE JIJINI ARUSHA.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini Profesa James Mdoe ametembelea mnada wa Madini ya Tanzanite yaliyochimbwa kutoka migodi ya Kampuni tano za wafanyabiasha wa madini hayo ili kuona utaratibu unaotumika kuwapata washindi wa zabuni za kununua madini ya hayo wakati wa mnada.

Mnada huo unatarajia kufanyika Agosti 12 mwaka huu na unafanyia Tanzania kwa mara kwanza; Vilevile watakaoshinda zabuni za kununua madini ya hayo watatangazwa wakati wa mnada.Mnada huo umeshirikisha wafanyabiashara wa Madini wa ndani na nje ya Tanzania. 
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe ( kushoto) akionyeshwa namna ya kutambua ubora wa jiwe la Tanzanite na Mkurugenzi wa Uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo( kulia).