Tuesday, August 16, 2016

MBUNGE WA MKURANGA,MH. ULEGA AKABIDHI MADAWATI 537 HALMASHAURI YA WILAYA YA MKURANGA.

Mbunge Abdallah Ulega (katika alie simama) akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Msham Munde, mkuu wa wilaya hiyo Filberto Sanga, na mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke mara baada ya kukabidhi madawati 537 ya mbunge wilayani humo.Sehemu ya madawati ya hayo. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii) 
Mbunge wa Jimbo mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Njopeka mara baada ya kufanya ziara ya kuwashukuru wananchi hao baada ya kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo ambapo pia mbali na kushukuru anatumia mikutano hiyo kuhamasisha maendeleo na kuwataka kufanya kazi kwa bidii leo mkoani Pwani.
Walimu wa shule ya msingi Misasa wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega mara baada ya kuzuru shuleni hapo kwa lengo la kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii na kwamba yeye kama kiongozi wao yupo pamoja nao .
Akina mama wa kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Likanga wakimsilikiliza mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwa makini wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru uliofanyika kijiji hapo ambapo pia walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zao hususani kukosekana kwa Zahanati na maji safi. 
Watendaji wa halmashauri wakimsikiliza kwa makini mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega,katika mkutano wake wa hadhara wa kushurukuru wananchi wa kijiji cha Njopeka ,kata ya Likanga ambapo katika ziara hizo amekuwa akitembea na watendaji hao ili kujibu hoja mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwasili katika kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Lukanga ,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa kijiji waliokuja kumpokea,ulega yupo katika ziara ya kushukuru wananchi wake pamoja na kuhamasisha maendeleo ya watu.
Mbunge Abdallah Ulega akikabidhi madawati 537 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mkuranga Msham Munde ,madawati hayo yametokana na fedha zilizotolewa na bunge baada ya kubana matumizi na kukabidhiwa Rais Dkt John Magufuli ambaye naye aliagiza zitengeneze madawati.
Mdau wa maendeleo kutoka kampuni ya Hamisi Njomoke Limited akimkabidhi madawati 50 mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kauli mbiu ya rais ya kuwataka watanzania kujitokeza kuchangia ili kuondoa kero hiyo katika shule leo mokani Pwani.

AWATAKA VIONGOZI NA WALIMU KUTUZA MADAWATI HAYO 

Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi madawati 537 kwa halmashauri ya wilaya hiyo, huku akiwataka viongozi wakiwamo madiwani wa kata mbalimbali kusimamia vizuri madawati hayo ili kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi alisema kuwa madawati hayo yametokana na fedha zao ambazo zilibaki baada ya kubana matumizi katika ofisi ya bunge na kwa kauli moja walikubali kumkabidhi Rais Dkt. Magufuli, ambapo naye kwa kutambua changamoto ya madawati akaelekeza fedha hizo zipelekwe kutengeneza madawati hayo. 

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msham Munde alimshukuru Mbunge huyo na kudai kuwa uchangiaji wa madawati hayo ni mchakato endelevu hivyo wadau waendelee kujitokeza kuchangia huku akisisitiza kwamba kwa asilimia kubwa yamekwenda kutatua kero hiyo. 

Wakati huohuo mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke alimkabidhi mbunge wa jimbo hilo Ulega Madawati 50 kama sehemu ya kumuunga mkono mbunge paoja na Rais Dkt Magufuli huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia ili watoto wasome katika mazingira rafiki.

No comments:

Post a Comment