Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake alfajiri ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.
Na huko mkoani Kigoma Jeshi la Polisi liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.
