Thursday, August 11, 2016

WARATIBU WA MIRADI YA MAENDELEO TEMEKE WATAKIWA KUCHORA RAMANI YA MAENEO YA MRADI- HASSAN

 Mhandisi kutoka kampuni ya Kyondonga ya nchini Korea, Lee akielezea mradi wa maendeleo wa uboreshaji wa miundo mbinu ambapo wameingia mkataba na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikishirikisha jumla ya kata 13.

Mratibu wa Mradi wa maendeleo wa uboreshaji wa miundombinu, Edwars Saimon akizungumza na wadau kutoka taasisi mbalimbali jijini Dar es Salaam leo. Mstahiki Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa wa Temeke, Feisal Hassan.
 Katibu Tawala Manispaa ya Temeke, Hashim Komba akitoa ufafanuzi kuhusiana na masuala mbalimbali wakati wa uchangiaji wa hoja ya mradi wa maendeleo ya uboreshwaji wa miundombinu wilaya ya Temeke.
Wadau na wawakilishi mbalimbali kutoka taasisi binfasi na za umma wakiwa katika kikao cha pamoja na halmashauri ya manispaa ya Temeke wakiongozwa na Mstahiki Naibu Meyawa Manispaa ya Temeke, Feisal Hassana katika mradi wa maendeleo wa uboreshaji wa miundo mbinu uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

NAIBU Mstaiki meya wa Manispaa ya Temeke amewataka waratibu wa mradi wa Maendeleo wa uboreshaji wa miundombinu ya Manispaa hiyo kuweka wazi maeneo yatayopitiwa na mradi  na kuchora ramani zinazoonesha mapito ya mradi huo.


Mradi wa maendeleo wa uboreshaji wa miundo mbinu utajumuisha kata 13 za Manispaa hiyo ukilenga zaidi masoko, zahanati, barabara pamoja na daraja la Kijichi Tuangoma. 

Hayo ameyasema Mstahiki Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Feisal Hassan wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa taasisi za Serikali na binafsi jijini Dar es Salaa leo, Amesema kuwa hatua hii itaboresha manispaa ya Temeke kwa ujumla ikiwemo katika kupata zahanati, masoko na barabara bora.

Amesisitiza kuwa watakaokwamisha mradi huu watawajibika moja kwa moja na watapelekwa kwa Waziri Mkuu kwa maelezo zaidi kwani tunataka mabadiliko ndani ya Temeke na hilo linawezekana. 

Naye mratibu wa mradi huo Edward Saimon amesem Kuwa mpaka kufikia Desemba 31 watakuwa wameshapata mchoro mzima na namna uboreshwaji wa miundo mbinu utakavyokuwa.

Saimon amesema kuwa katika kuhakikisha wananchi wanalipwa fidia zao mchakato wa kuendelea kuhakiki majina mengine unaendelea.

Kata zitakazopitiwa na mradi huo ni Kijichi, Mbagala Kuu, Temeke, Kilakala, Keko, Makangarawe, Mtoni, Yombo Vituka , Sandali, Chang'ombe, Azimio na Kata 15.

No comments:

Post a Comment