Showing posts with label Waziri wa Nishati na Madini. Show all posts
Showing posts with label Waziri wa Nishati na Madini. Show all posts
Tuesday, August 16, 2016
Saturday, August 06, 2016
Thursday, August 04, 2016
WAZIRI MHONGO ATEMBELEWA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA.
BALOZI wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi zao hususan katika sekta ya nishati.
Balozi Yoshida, aliyeambatana na Ujumbe wa baadhi ya maofisa kutoka Ubalozini na wataalam kadhaa kutoka Shirika la Japan Oil, Gas and Metals National Corporation (JOGMEC), alimtembelea Prof Muhongo Agosti 3 mwaka huu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida (Kulia kwa Waziri) na Ujumbe wake, walipomtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Monday, April 25, 2016
WAZIRI MUHONGO AWASILI JIJINI DAR AKITOKEA NCHINI UGANDA KUKAMILISHA DILI LA BOMBA LA MAFUTA:
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam jioni hii, akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo.
Friday, April 08, 2016
PROFESA MUHONGO ASISITIZA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KATIKA SEKTA YA NISHATI NA MADINI.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhungo akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kufungua baraza la wafanyakazi wa wizara yake katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la wafanyazaki wa wizara ya Nishati na Madini, Selina Msumbushi akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kusoma mapendekezo ya wafanyakazi hao leo katika mkutano wa kufungua baraza la wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)


