Friday, August 05, 2016

IDARA YA UHAMIAJI INAWASHIKILIA WATUMISHI WAWILI WA SERIKALI AMBAO SI RAI WA TANZANIA.

Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa Serikali ambao sio raia wa Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa ambao sio raia wa Tanzania waliokuwa wakifanya kazi serikalini wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa Uhamiaji, kushoto ni Bw. Bahilanya Milingita aliyekuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)na kulia ni Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba ambaye alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya Mburahati.

Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo ambaye anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kinyume na sheria za nchi.

Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi ambaye alikuwa Mganga Mkuu katika kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa kufanya kazi Serikalini wakati si raia wa Tanzania.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa Serikali ambao sio raia wa Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment