Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisoma kipeperushi cha Mpango wa Pili wa Maendeleo
wa Miaka Mitano alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho
ya Wakulima Nanenane Mkoani Lindi.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) na Mke wa Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete (wa pili
kulia) wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Kilimo walipotembelea banda la
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika Maonesho ya wakulima (Nanenane) katika viwanja
vya Ngongo-Lindi.
Wananchi
kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusu maonesho
ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Alexander Lweikiza, alipotembelea banda la Wizara hiyo katika Maonesho
ya Wakulima Nane nane Mkoani Lindi.
Mkuu
wa Hazina Ndogo Mkoani Lindi Bi. Pili Kamali (wa pili kulia) pamoja na wakazi wa
mkoa wa Lindi wakipata maelezo kwa mtaalamu wa Taasisi iliyochini ya Wizara ya Fedha
na Mipango katika Maonesho ya Wakulima Nane nane Mkoani Lindi.
Walimu wa
Sekondari Mnolela iliyopo Mkoani Lindi wakipata maelezo katika Taasisi ya
Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA) walipotembelea katika banda la Wizara
ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea
katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Walimu na
wanafunzi wa Sekondari ya Mnolela Mkoani Lindi wakipata maelezo kutoka kwa
mtaalamu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) walipotembelea katika banda la
Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane
yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Walimu na
wanafunzi wa Sekondari ya Mnolela Mkoani Lindi wakipata maelezo kutoka kwa
mtaalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu Hotuba ya Bajeti Kuu ya mwaka
2016/2017 walipotembelea katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika
Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani
Lindi.
RC ZAMBI AITAKA WIZARA YA FEDHA KUJENGA MIUNDOMBINU YA KUDUMU ENEO LA NANE NANE-NGONGO
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake kujenga jengo la kudumu katika Viwanja vya maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane) mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo ili kupunguza gharama za kukodi maturubai wakati wa maonesho.
Alisema pamoja na kupunguza gharama, baada ya maonesho, jengo hilo linaweza kutumiwa katika shughuli nyingine na Halmashauri ya Wilaya hivyo kuiongezea Wizara kipato.
Mhe. Zambi alitoa ushauri huo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika viwanja vya Ngongo Lindi ambapo aliweza kuona shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanyika katika mabanda ya yanayotumiwa na Taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo.
Vilevile alizishauri Taasisi kujitangaza ili wananchi wengi waweze kufahamu huduma zinazotolewa na Taasisi hizo kwani huduma zao ni muhimu kwa Wananchi hususani wakulima.
"Wananchi wengi wanaoishi mikoani hususani Lindi, hawana uelewa wa kutosha kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi zilizo chini ya Wizara hasa huduma ya Bima na Mifuko ya uwekezaji"Alisema Zambi.
Alisema kuwa maonesho haya yanawawezesha Wananchi kuelewa pia namna ya utekelezaji wa bajeti na vipaumbele vyake kamavile kujenga miundombinu ya Barabara, Maji, Elimu na Afya.
Mhe. Zambi ameziomba Taasisi zinazoshughulika na utoaji mikopo kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini hasa wakulima ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
Pia aliipongeza Serikali kwa kuandaa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao anaamini utakua chachu ya mapinduzi ya kiuchumi kwani mpango huo umelenga zaidi katika kukuza viwanda ambayo vitaongeza ajira kwa vijana.
Pia alitoa rai kwa Taasisi ambazo hazijashikiri maonesho hayo mwaka huu kujipanga kwa ajili ya mwakani kwani maonesho hayo ni muhimu kwao, Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
No comments:
Post a Comment