MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amewataka madiwani na watendaji kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo na kwamba muda wa kufanya siasa umemalizika na kilichobaki ni kuchapa kazi kama Rais Dkt. John Magufuli anavyohamasisha kwamba watu wafanye kazi.
Ulega ametoa kauli hiyo leo katika semina ya madiwani na watendaji kata pamoja na wataalamu wa afya kutoka halmashauri juu ya masuala mazima ya usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo na kudai kuwa wilaya ya Mkuranga kuna changamoto ya watu tabia ya kutumia vyoo hali inayojenga taswira mbaya wilayani humo.
Alisema kuwa wilaya hiyo inachangamoto kubwa ya watu kushindwa kutumia vyoo na kujenga taswira mbaya katika jamii hivyo lazima watu wajenge tamaduni ya matumizi ya vyoo nakutoa elimu hiyo kuazia utotoni ili hata mtoto anapokuwa anakuwa tayari na uelewa juu ya matumizi ya vyoo.
Injia wa Maji ndani ya Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Leonard Baseke akitoa ufafanuzi juu ya matumizi bora ya vyoo kwa wananchi wa wilaya hiyo katika semina iliyoshirikisha madiwani na watendaji kata wa wilaya ya mkuranga leo mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na madiwani pamoja na watendaji kata ndani ya wilaya ya Mkuranga mara baada ya kutoka kwenye semina ya uhamasishaji wa usafi hususani baada ya kutoka chooni.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza katika semina ya iliyoshilikisha madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka madiwani hao na watendaji kata ndani ya wilaya hiyo kufanya kazi nakuacha siasa kwani muda wake umekwisha leo mkoani Pwani.
Madiwani wa halmashauri hiyo na watendaji kata kwa pamoja wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalla Ulega wakati akizungumza katika semina ya kuhamasisha masuala ya usafi na matumizi ya vyoo ikiwa pamoja na kujenga tabia ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni leo mkoani Pwani.
Picha na Emmanuel massaka, Globu ya Jamii, Mkuranga
No comments:
Post a Comment