Tuesday, April 05, 2016

WAAJIRI WA SERIKALI WAAGIZWA KUWASILISHA TAARIFA ZAO WAAJIRIWA WAO NDANI YA WIKI HII.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusiana na Watumishi walioondolewa katika Orodha ya Malipo ya Mishahara (payroll).
 Katibu Mkuu-Utumishi  Dkt. Laurean Ndumbaro na Kushoto ni Naibu katibu Mkuu -Utumishi, Suzan  Mlawi  wakimsikiliza  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki jijini Dar es Salaam .

Na Anaseli Stanley.
WAAJIRI wa Serikali waagizwa kuwasilisha taarifa zao waajiriwa wao ndani ya wiki hii ili kuwezesha Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma, kujua kwa usahihi watumishi wangapi ni hewa na hatua ziendelee kuchukuliwa.

Haya yameagizwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa taarifa za  Machi 1 hadi April 4 mwaka huu zinaonyesha watumishi 4,317 waliondolewa katika Payroll ya Serikali ikiwa ni kasi ya kuondoa watumishi ambao utumishi wao umekoma kwa kipindi kifupi ambapo haijawahi kufikiwa kwa kipindi cha nyuma ikiwa ni mwitikio wa agizo la Rais Dkt Magufuli.

"Kutokana na Mfumo wa HCMIS ambao hufungwa kila tarehe 5 ya kila mwezi umewezesha Watumishi wa Serikali 1,284 kufutwa kwa Aprili 1 hadi 4 ikiwa imejumuishwa watumishi hewa, waliostaafu, walioacha kazi waliofukuzwa na waliofariki dunia"Amesema Angela.

 Angela amesema kuwa muda wa kufunga Payroll umeongezwa na utafungwa Aprili 12 ili kuhakiki watumishi wote wa serikali ambao hawastahili kuwepo kwenye Payroll" 

Pia amesema kuwa baada ya tarehe hiyo Ofisi yake itafanya ukaguzi kwenye taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali ili kuhakikisha wale ambao hawawajibiki au kutimiza wajibu wao katika eneo la usimamizi wa rasilimali watu wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment