Kampuni ya Kijapani inayofanya shughuli zake
nchini (Tricster) imeandaa shindano la
wazo la biashara litakalozishirikisha nchi tano
za Afrika zikiwemo Kenya,Rwanda,Zambia,Zimbabwe na Tanzania mwenyeji
wa mashindano hayo kwa mwaka 2016.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New Business Development
Department(DMM) Bw.Alex Kapungu ambao
ndio wadhamini wa shindano hilo ameeleza
kuwa lengo la shindano hilo ni kusaidia
kuboresha ujasiriamali katika bara la Afrika.
“Shindano hili linafanyika kwa mara ya kwanza na
hivyo ni fursa nzuri kwa wajasiriamali na wale wanaotaka kuwa wajasiriamali
kushiriki na baadaye kufanikisha wazo hilo kiutendaji kwa kuwa biashara halisi”alisema
Bw.Alex.
Aidha ameongeza kuwa vigezo vya kushiriki shindano
hilo ni mshiriki awe amefikisha miaka 18 na kuendelea, awe anajua kuongea na
kuandika lugha ya kiingereza na kuwa na hati ya kusafiria.
Naye Mkurugenzi wa Trickster Bw.Sonobe Atsushi
amesema washindi watakaoingia nusu fainali watapata fursa ya kutembelea nchi ya japani ambapo mshindi
wa kwanza atapata fedha taslimu Dola
elfu tano za kimarekani.
Pia ametoa wito kwa watanzania kujitokeza na
kushiriki kwa wingi ili wapate fursa ya kuanzisha biashara kupitia mawazo
watakayoyatoa na hivyo kupanua wigo wa biashara.
No comments:
Post a Comment