Tuesday, April 12, 2016

MAKONGORO NYERERE AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO AFRIKA MASHARIKI


 Mwenyekiti wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (Katikati) akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu program ya bunge hilo ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa jumuiya hiyo ili kupata fursa mbalimbali, kulia ni mbunge wa bunge hilo Mhe. Abdulah Mwinyi na kushoto ni Mhe. Shyrose Bhanji.

 Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdulah Mwinyi (katikati) akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa Watanzania kuwa mstari wa mbele katika kutafuta taarifa kuhusu fursa za mtangamano wa Afrika Mashariki, kulia ni Mhe. Bernard Murunya (MB) na kushoto ni Mwenyekiti wa wabunge hao Mhe. Makongoro Nyerere.
  Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Adam Kimbisa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki walipokuwa wanaelezea program ya bunge hilo ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa jumuiya.
 Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki walipokuwa wanaelezea program ya bunge hilo ya kuhamasisha wananchi katika kutafuta taarifa kuhusu fursa za mtangamano wa Afrika Mashariki, kulia ni Mwenyekiti wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere na kushoto ni Mhe. Maryam Ussi Yahya.
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Bernard Murunya akisistiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuhusu program ya bunge hilo ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa jumuiya hiyo, kushoto ni Mhe. Abdulah Mwinyi.
 Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Maryam Ussi Yahya akifafanua jambo kwa waandishi wea habari (hawapo pichani) kuhusu program ya bunge hilo ya kuhamasisha wananchi katika kutafuta taarifa kuhusu fursa za mtangamano wa Afrika Mashariki, kulia ni Mbunge wa Bunge hilo Mhe. Shyrose Bhanji na kushoto ni Mhe. Nderakindo Kessy.
 Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Nderakindo Kessy (aliyesimama) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu program ya bunge hilo ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa jumuiya hiyo,toka kulia waliokaa ni Mhe. Abdulah Mwinyi, Mwenyekiti wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (Katikati) na Mhe. Shyrose Bhanji.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini taarifa iliyotolewa na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (hawapo pichani) kuhusu program ya bunge hilo ya kuhamasisha wananchi kuhusu mtangamano wa jumuiya hiyo.

Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo

Wananchi wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia nafasi za kufanya baishara zilizopo kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo makubaliano ambayo yanawapa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara kwa uhuru.

Hayo yalisemwa jana na Mbuge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere ambaye alidai kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho wa kisiasa.

Alisema kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya baishara katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya kusambaza bishaa zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Huu ni muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya baishara kwa nchi za Afrika Mashariki, vikwazo zilivyopo kwa sasa ni wananchi wengi wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo lakini tumejipanga katika hilo,” alisema Nyerere.

Alisema kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na ushirikiano huo.

Alisema programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu, vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la Feri.

Pia Nyerere aliwataka Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa mbalimbali kupitia mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na fursa nyingi ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.

No comments:

Post a Comment