Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.
George Simbachawene (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuia ya
Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw. Johnsen Estomih Minja mara baada ya kikao
chao jijini Dar es Salaam.
Na Rebecca Kwandu, TAMISEMI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene amekutana na viongozi
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania na kupata nafasi ya kusikiliza kero
mbalimbali zinazowakabili na kuahidi kushirikiana nao katika kutatua kero hizo.
Akizungumza
na wafanyabiashara hao waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam
katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Tamisemi wamejadiliana masuala mbalimbali ya
kibiashara ili yaweze kunufaisha jamii na taifa.
“Nimesikia
mapendekezo yenu nitayafanyia kazi, nitawaita ili tujadiliane katika kujenga
mazingira bora na rafiki ya biashara yatakuwa na manufaa kwenu taifa kwa ujumla”
alisema Mhe. Simbachawene.
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa
dhati kushirikiana na wafanyabiashara nchini na kulihakikishia taifa kuwa
uchumi imara kulingana na Dira ya
Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
Katika
kikao hicho wafanyabiashara walipata nafasi ya kumueleza Mhe. Waziri kero
mbalimbali zinazowakabili zikiwepo utitiri wa kodi, ugumu katika upatikanaji wa
leseni na kukosekana kwa uwiano wa tozo za leseni kati ya sehemu moja na
nyingine ambapo Mhe. Waziri aliahidi kufanyia kazi kero na mapendekezo
mbalimbali ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara waliyowasilisha kwake.
Akizungumza
katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw.
Johnsen Estomih Minja alisema wafanyabiashara wanapenda kuona Tanzania ikikua
kiuchumi na wao kama wafanyabiashara wangependa kuwa wadau wa kuisaidia nchi
kukua kiuchumi, hivyo wanaomba serikali iweze kuwashirikisha katika masuala
mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kibiashara ili waweze kutoa mchango wao
wa mawazo na kuondoa ugomvi kati ya wafanyabiashara na Serikali yao.
Miongoni
mwa masuala ambayo Jumuia ya
Wafanyabishara Tanzania imependekeza yaangaliwe kwa undani kuwa ni pamoja na
serikali kuangalia upanuzi wa wigo wa ulipaji wa kodi,kuunganishwa kwa kodi na
tozo mbalimbali katika ulipaji na
kurahisishwa kwa utaratibu wa ulipaji wa leseni.
No comments:
Post a Comment