Showing posts with label Mhe. George Simbachawene. Show all posts
Showing posts with label Mhe. George Simbachawene. Show all posts

Monday, April 18, 2016

TAASISI YA GRACA MACHEL MDAU MUHIMU WA ELIMU YA MTOTO WA KIKE NCHINI, IKIWA NA LENGO LA KUIELIMISHA JAMII.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Mtoto huanza kujifunza kulingana na mazingira yake yanayomzunguka, mafunzo hayo yanamuwezesha kupata uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile ili aweze kuyamudu mazingira yake.
Hali hiyo inajenga dhana ya kupata elimu kulingana na mazingira ambayo hujulikana kama elimu isiyo rasmi.
Ni vema ikaeleweka kwamba tunapozungumza kuhusu watoto, tunazikusudia jinsia zote mbili, yaani watoto wa kike na wale wa kiume. Katika hali halisi ndani ya maisha ya kijamii, elimu ni nyenzo ambayo hutumiwa kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine bila kujali jinsia.
Elimu kwa watoto wa kike ni moja ya njia bora za kupunguza umaskini katika mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania.
Manufaa hayo ya elimu kwa watoto wa kike yanaweza kuonekana kwa mtu binafsi, familia zao, jamii yote na taifa kwa ujumla.
Ni dhahiri, manufaa yanayopatikana kupita elimu ni mengi katika jamii ikiwemo kupunguza idadi ya watoto ambao wanawake hujifungua, kupunguza idadi ya vifo vya watoto wadogo, kupunguza idadi ya vifo vya akina mama, kuwalinda dhidi ya maambukizo ya VVU/UKIMWI na kuongeza idadi ya wanawake wenye kazi na mapato ya juu ambayo hudumu kwa vizazi vingi.
Hakika ukimuelimisha mtoto wa kike, umemsaidia kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa manufaa yake, familia yake na hata taifa.
Hali hii imechukua sura mpya nchini Tanzania ambapo Serikali, watu binafsi, mashirika ya dini   na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi zimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu ambayo ndiyo kinga na urithi pekee ambao hawezi kunyang’anywa wala kugawana na mtu mwingine ndani ya familia na hata jamii inayomzunguka.
Sura hiyo mpya imeoneshwa na Mfuko wa Graca Machel (Graca Machel Trust) ambao umejikita katika kusaidia wanawake na watoto nchi kadhaa Barani Afrika.

Saturday, April 16, 2016

MEI KUMI MABASI YAENDAYO KASI KUANZA KAZI:


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu. 

Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara ya Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Simbachawene alisema baada ya kukutana na wadau wa mradi huo, wamewahakikishia kuwa utaanza rasmi mwezi ujao bila kukosa. 

“Tumeambiwa mradi huu una mikataba mingi na kuwa bado kuna mjadala mkubwa wa mikataba. Hatuwezi kulazimisha maana unaweza kujikuta ukitengeneza mikataba mibaya, hivyo tunaendelea na mijadala ya mikataba,” alisema. 

Thursday, April 14, 2016

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS-TAMISEMI, GEORGE SIMBACHAWENE AVUNJA BODI YA MACHINGA COMPELEX:


Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amevunja bodi ya Soko la Machinga Complex lililopo Ilala Mchikini Dar es Salaam na kulikabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Thursday, April 07, 2016

WAFANYABIASHARA WAAHIDI USHIRIKIANO NA MHE. SIMBACHAWENE ALIPOKUTANA NAO:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiongea na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene jijini Dar es Salaam.

Wednesday, April 06, 2016

WATOTO WA KIKE 20,000 KUNUFAIKA NA MFUKO WA GRACA MACHEL MKOANI MARA.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene (kulia) akiongea na Mama Graca Machel (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene akiongea na Mama Graca Machel (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.