Showing posts with label Zambia. Show all posts
Showing posts with label Zambia. Show all posts

Tuesday, April 12, 2016

KAMPUNI YA KIJAPANI INAYOFANYA SHUGHULI ZAKE NCHINI (TRICSTER) IMEANDAA SHINDANO LA WAZO LA BIASHARA

Na Lorietha Laurence-Maelezo
Kampuni ya Kijapani inayofanya shughuli zake nchini (Tricster)  imeandaa shindano la wazo la biashara  litakalozishirikisha  nchi tano  za Afrika zikiwemo Kenya,Rwanda,Zambia,Zimbabwe na Tanzania mwenyeji wa  mashindano hayo kwa mwaka 2016.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Mradi kutoka kampuni ya Afrika New Business Development Department(DMM)  Bw.Alex Kapungu ambao ndio  wadhamini wa shindano hilo ameeleza kuwa lengo la shindano hilo ni  kusaidia kuboresha ujasiriamali katika bara la Afrika.