Askari polisi na wasamaria wema wakisaidia kutoa maiti kutoka katika basi la Lupondije Express namba T 798 AKV kutoka Mwanza - Iringa baada ya kupinduka eneo la Mteremko wa Ipogolo mjini Iringa usiku wa leo
Gari la kikosi cha Zimamoto na uokoaji likiwa eneo la tukio kusaidia kuokoa maisha ya majeruhi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kushoto akiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw Peter Kakamba wakisaidia kuokoa majeruhi na kutoa maiti
Gari la kikosi cha Zimamoto na uokoaji likiwa eneo la tukio kusaidia kuokoa maisha ya majeruhi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kushoto akiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw Peter Kakamba wakisaidia kuokoa majeruhi na kutoa maiti
WATU zaidi ya wane wakufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya baada ya basi lenye namba za usajili T 798 AKV mali ya Lupondije Express Kutoka Mwanza kuja Iringa kupinduka eneo la Mteremko wa Ipogolo mjini Iringa wakati basi hilo likielekea kufaulisha abiria wa Mbeya.
Imeelezwa kuwa baadhi ya abiria waliokufa katika ajali hiyo na majeruhi ni wale ambao walitakiwa kushuka stendi kuu ya mabasi ya mabasi yaendaye mikoani mjini Iringa ila dereva wa basi aligoma kuwashusha stendi na kupitiliza nao kwenda Ipogolo kufaulisha abiria wa Mbeya kwanza ndipo arudi kuwashusha stendi.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku baada ya basi hilo kufeli breki katika mteremko huo huo mkali kabla ya kupinduka .
Wema Zuberi ni mmoja kati ya majeruhi wa ajali hiyo aliyekuwa ametoka mkoani Dodoma kuelekea Mbeya aliueleza mtandao huu wa matukiodaima Blog kuwa mwendo wa basi hilo toka amepanda Dodoma kuja Iringa haukuwa mkali sana ulikuwa ni mwendo wa kawaida .
Japo alisema kuwa baada ya kuingia mjini Iringa katikati ya mji ndipo dereva wa basi hilo alionyesha kuendesha basi hilo kwa mwendo mkali zaidi kiasi cha baadhi ya abiria kulalamika mwendo huo na kutaka kushushwa ila dereva hakuweza kusikia zaidi ya kuwapuuza abiria hao.
“Abiria wengi walionyesha kumlalamikia dereva huyo kwanza kutokana na kuwapitiliza stendi pasipo kuwashusha na pili mwendo kasi ambao alikuwa akienda nao ili kufanikisha kutufaulisha abiria tuliokuwa tukielekea Mbeya “
Alisema kabla ya kufika eneo hilo ambalo basi lilipinduka kuna kona kali na mteremko mkali na kilichoonekana haraka haraka ni dereva kushindwa kukata kona hiyo baada ya Breki kufeli na hivyo kulazimika kuhama njia na kugonga kingo za barabara hiyo na kupinduka .
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema kuwa zoezi la kuendelea kutafuta miili iliyobanwa na basi hilo imekuwa ngumu kutokana na kukosekana kwa gari la kuinua basi hilo na tayari amemwagiza meneja wa Tanesco kuleta gari hilo na iwapo dereva hayupo basi kuamka na kuendesha mwenyewe .
Hata hivyo alisema kuwa kuanzia sasa dawa ya madereva hao ni kuwashughulikia kwani kama Rai imekwisha tolewa mara nyingi na bado ajali zinaendelea kutokea.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Bw Peter Kakamba ambae pia alikuwepo eneo la tukio kusaidia kuokoa majeruhi na kutoa maiti katika basi hilo pamoja na mkuu huyo wa wilaya wananchi mbali mbali walioongozwa na askari polisi ,alisema kuwa hadi majira ya saa 5 usiku wakati tunakwenda mitamboni bado ilikuwa ni mapema kuweza kujua ni watu wangapi wamepoteza maisha kwani zoezi lilikuwa bado linaendelea.
Kamanda huyo aliahidi kutoa taarifa mara tu zoezi hilo litakapokamilika kwa kuinua basi hilo na kutazama kwa kina kama kuna miili ambayo imefunikwa chini ama lah.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia miili minne ikiwa tayari imetolewa katika basi hilo huku majeruhi wengi wakiwa wamepata majeraha makubwa mikononi ,miguuni na kichwani,Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
No comments:
Post a Comment