Thursday, March 17, 2016

17.03. 2016.HII NI TAARIFA YA HABARI KUTOKA WAPO REDIO FM.


.NAIBU WAZIRI WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA WAZEE NA WATOTO DKT. HAMISI KIGWANGALA AMEWATAKA WAMILIKI WA MADUKA YA DAWA AMBAO HAWANA VIBALI KUYAFUNGA MADUKA YAO MARA MOJA.

CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMESEMA KUWA KUNA VITENDO VYA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU VINAENDELEA VISIWANI ZANZIBAR  HIVYO KIMETOA ONYO KWA SERIKALI KUDHIBITI VITENDI HIVYO.


.SHIRIKA MOJA LA KIMATAIFA LIMESEMA USHINDI WA DONALD TRUMP UNACHUKULIWA KUWA MIONGONI MWA HATARI 10 KUU ZAIDI ZINAZOIKABILI DUNIA.
.MAAFISA WA SERIKALI YA SOMALIA NA JESHI LA KENYA WAMESEMA WAPIGANAJI 30 WA AL-SHABAAB WAMEUAWA KATIKA MASHAMBULIO MAWILI TOFAUTI.


HABARI KAMILI.
Naibu waziri wizara ya Afya Maendeleo ya jamii ,jinsia wazee na watoto Dkt. Hamisi Kigwangala amewataka wamiliki wa maduka ya dawa ambao hawana vibali kuyafunga maduka yao mara moja.

Akizungumza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Dkt. Kigwangala amesema tamko hilo limetokana na operesheni safisha katika maduka ya dawa muhimu katika mikoa tisa na kubainika kwa ukiukwaji wa sheria katika maeneo ya uendeshaji wa huduma hizo.

Dkt. Kigwangala amewataka watendaji wa sekta ya afya ngazi za mikoa .manispaa, halmashauri za wilaya na miji kuhakikisha wanafunga na kuyaondoa maduka yote ya dawa bubu ambayo hayana vibali vya usajili na yanayo endeshwa kinyume cha sheria.

NA JESCA MATHEW




Imeelezwa kuwa watumishi wengi wa serikali bado hawana elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya afya itakayowawezesha kupata matibabu hata baada ya kustaafu.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa bima ya safya NHIF Bwa. Emanueli Luhumba alipokuwa akizungumza na wastaafu ambao ni wanachama wa mfuko huo amesema bima hiyo itamwezesha mtumishi wa serikali kutoa angaika na na fgharama za matibabu wakati anapoumwa hasa akistaafu.
Bwa. Luhumba ameongeza kuwa serikali itaendelea kutroa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu mifuko ya bima ya afya ambapo serikali inadhamiria kuboresha mfuko huo ili iwezekuhudumia watu wengi zaidi.



NA SHIVA MGIMBA. 




Chama cha wananchi CUF kimesema kuwa kuna vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vinaendelea Visiwani Zanzibar  hivyo kimetoa onyo kwa serikali kudhibiti vitendi hivyo.
Hayo yamesemwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho bara Mh. Magdalena sakaya wakati akizungumza jijini Dar es salaam katika ofisi za chama hicho ambapo amesema Zanzibar kumekuwa na vikundi viovu maarufu kama mazombi.
Ameongeza kuwa zaidi ya wafuasi 60 wa CUF wamekamatwa wakitajwa kuhusika na uvanjifu wa amani ambapo ajanuari mwaka huu chama cha cuf kilitoa msimamo wake wa kutoshiriki uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika marcha 20, mwaka 2016.




NA. HAPPY GOMEZULU.



Shirika la kimataifa linalo saidia watoto la Save the Children limekuwa likifanya jitihada mbalimbali katika kuelimisha jamii kuhusu ndoa za utotoni na ukandamizaji unaosababishwa na  baadhi ya mila za makabila  hapa nchini.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na shirika hilo  mkurugenzi   wa kituo cha  Baba  watoto centre  Mgunga Mwamnyenyelwa amesema  Jamii ,wapigania haki za watoto na taasisi  za serikali wanapaswa kushirikiana  kwa pamoja  katika kuliondoa  tatizo hilo.

Kwaupande wake mkurugenzi msaidizi wa maendeleo  ya mtoto wizara ya  Afya  maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Benedict Missani amesema tatizo la ndoa za utotoni ni kubwa hasa katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Shiyanga.





NA JOHN LUHENDE



UNAENDELEA KUSIKILIZA TAARIFA YA HABARI KUTOKA WAPO RADIO FM.

Shirika moja la kimataifa limesema ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa miongoni mwa hatari 10 kuu zaidi zinazoikabili dunia.
Shirika hilo la Economist Intelligence Unit linaonya kuwa iwapo Bw Trump atashinda urais Marekani huenda ushindi huo ukavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani.
Ushindi wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kuliko Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya kivita katika bahari ya South China Sea.












Wanachama 89 wa kundi la Kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria wamehukumiwa kifo nchini Cameroon baada ya kupatikana na makosa ya kujihusisha na ugaidi.
Wanachama hao wamehukumiwa na mahakama ya kijeshi kwa mchango wao katika mashambulio kadha eneo la kaskazini mwa Cameroon mpakani na Nigeria ambapo eneo hilo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Boko Haram.
Waliohukumiwa ni sehemu ya wanachama 850 wanaozuiliwa nchini Cameroon kwa kudaiwa kuhusika na mashambulio ya kundi hilo la Kiislamu ikiwa ni mara ya kwanza kwa watu kuhukumiwa kifo chini ya sheria mpya za kukabiliana na ugaidi zilizopitishwa mwaka 2014.











Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanya majaribio ya silaha za nyuklia na makombora hivi karibuni.
Msemaji wa ikulu ya White House amesema Marekani na jamii ya kimataifa hawatavumilia shughuli haramu za nyuklia zinazotekelezwa na Korea Kaskazini.

Kauli hiyo inakuja baada ya Korea Kaskazini kumhukumu mwanafunzi Mmarekani kifungo cha miaka 15 na kazi ngumu jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola.













Maafisa wa serikali ya Somalia na jeshi la Kenya wamesema wapiganaji 30 wa al-Shabaab wameuawa katika mashambulio mawili tofauti.
Maafisa wa serikali katika jimbo la Puntland wanasema wapiganaji 11 waliuwawa walipojaribu kushambulia katika pwani ya nchi hiyo ambapo Gavana wa mkoa wa Nugal katika jimbo la Puntland, ambako mapigano yalitokea, amesema wapiganaji wengi wa al-Shabaab walijaribu kushambulia pwani ya Puntland.
Jeshi la Kenya limesema wapiganaji walijaribu kushambulia kambi za wanajeshi wa Kenya na Somalia usiku wa kuamkia Jumatano lakini wakakabiliwa vikali karibu na mji wa Afmadhow.


No comments:

Post a Comment