Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo kinyume na sheria.
Mmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa
Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya
kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha
uendeshaji na mfamasia husika.
Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa
Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine,
ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa
mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka
kama hilo.
Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la
kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani
mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.
Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali,
Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai
kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia
ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya
kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa
binadamu n ahata kumsababishia matatizo.
Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche
kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu
ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi
zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia
mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa
milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi
hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima
kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha
kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.
No comments:
Post a Comment