Chama cha Mapinduzi CCM leo kimemtangaza Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji wa CCM .Sendeka ametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar.Akimtangaza leo,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amesema kuwa Sendeka atafanya kazi zake chini ya Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnaye,amesema ,CCM imefanya uamuzi huo ili kumuwezesha Nape kutekeleza majuku yake vizuri ya Uwaziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo. Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnaye
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM , Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Ole Sendeka akizungumza baada ya kuteuliwa. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Picha: Bashir Nkoromo)TAARIFA ILIYOSOMWA NA OLE SENDEKA BAADA YA KUTAMBULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO.
Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.
Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.
CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.
No comments:
Post a Comment