Thursday, March 17, 2016

WIZARA YA AFYA,YAZINNDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA DAWA,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI HASA KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Bw.Mpoki Ulisubisye akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango kazi wa Taifa wa dawa,vifaa tiba, na vitendanishi hasa katika ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kudhibiti wizi wa dawa pamoja na uwajibikaji,mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde akifafanua jambo kwa waAndishi wa habari jinsi ya kuwezesha udhibiti wa wizi wa dawa pamoja na uwajibikaji, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).

Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imezindua mpango mkakati wa Taifa wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi hasa katika ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kuboresha huduma ya afya katika Halmashauri hizo.

Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Bw.Mpoki Ulisubisye amesema kila dawa katika Halmashauri husika itakuwa na nembo pamoja na takwimu za watumiaji kwa lengo la kukwepa wizi wa dawa na kuwapa taarifa wawekezaji kwa kuweka viwanda vya dawa za binadamu.

Katibu Mkuu huyo,Bw.Ulisubisye ameongeza kuwa ukaguzi wa dawa utakuwa endelevu,usimamizi wa vifaa pamoja na kuona utoaji wa huduma za afya kwa mpango huo una ubora mkubwa.

Hata hivyo, Wizara ya Afya imeeleza kuwa mpango huo utadumu kwa miaka mitano hasa katika kutekeleza mpango wa dawa kupatikana katika kila Halmashauri pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watoaji huduma za afya.

No comments:

Post a Comment