Mwenyekiti wa Madaktari bingwa wa ugonjwa wa Moyo, Robart Mvungi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusia na mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Aprili 21 na 22 mwaka huu, Amesema kuwa Mkutano huo utakuwa kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa wa Moyo ambao sio wa kuambukizwa.
Pia amesema kuwa mkutano huo utahudhuliwa na Madaktari bingwa ugonjwa wa moyo pia watatumia muda huo kuelimisha jamii ili kuweza kupunguza ongezeko la ugonjwa wa moyo hapa nchini.
Kushoto ni Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete, Ruben Muta, Mwaandaaji wa mkutano, Adeline Ndesanja na Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete,Tulizo Sanga.
Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete,Tulizo Sanga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari( hawapo pichani) jijini Dar es Salaam .
No comments:
Post a Comment