Kaimu Katibu
Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf
Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar
es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na Uzinduzi wa Mfumo wa Udahili wa
Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza
kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga
na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza
(“Bachelor Degree) wapili kushoto ni Mkuu wa Kitengo
cha Udahili Seremani Majindo, Mkurugenzi wa Mfumo na Upimaji,Bakari Issa
na Kaimu Mkurugenzi Idara ya vyuo na ushauri na Mipango.Uzinduzi
huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limetangaza ufunguzi rasmi
wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo
yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika
kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada
(Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree”).
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maelekezo na Msaada
kwa Taasisi wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga amesema kuwa, kwa mwaka wa masomo
wa 2015/16, Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa
kozi za astashahada (Cheti) na stashahada (Diploma) kwa mafunzo ya afya na
ualimu yaliyoidhinishwa na Baraza. ameongeza kuwa, Baraza pia
lilishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, kuratibu udahili wa wanafunzi
katika vyuo mbali mbali kwa kozi za shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili
wa Pamoja (Central Admission System (CAS)).
“Mifumo hii miwili ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha
waombaji kudahiliwa. Mifumo hii ya udahili imekuwa na mafanikio yafuatayo:
Kudhibiti udanganyifu katika udahili uliotokana na baadhi ya waombaji kutumia
vyeti vya bandia, kuwapunguzia waombaji gharama za kuomba udahili katika vyuo
mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mwombaji udahili mmoja kudahiliwa zaidi ya
mara moja na kuwanyima waombaji wengine nafasi, kuiwezesha serikali kuwa na
takwimu sahihi za waombaji udahili kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu
nchini, na kuwawezesha waombaji udahili kujiunga na mafunzo kwenye taasisi
zinazotambuliwa na Serikali,” alieleza.
Dk Rutayuga alieleza kuwa, kwa kutambua mafanikio ya udahili wa
pamoja yaliyopatikana, Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeamua kuwa maombi yote ya udahili
kwa ajili ya mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya
kwanza (Bachelor Degree) yafanywe kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili
(CAS).
Amefafanua kwamba. Baraza linautangazia umma kuwa, kuanzia mwaka wa
masomo 2016/2017 udahili wa kozi zote nchini utafanywa kupitia Mfumo wa Udahili
wa Pamoja (CAS) unaosimamiwa na NACTE, Vyuo Vikuu na taasisi za Elimu
zote nchini Tanzania zinazotoa mafunzo ya Cheti na Diploma kutodahili wanafunzi
nje ya mfumo wa udahili wa Pamoja kuanzia mwaka wa masomo 2016/17.
“Tunapenda kutoa taarifa pia kuwa, maombi ya kujiunga na kozi za Cheti
na Diploma yataanza kupokelewa rasmi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia
tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana. Baraza pia litaanza kupokea rasmi maombi
ya kujiunga na kozi za Shahada (Degree) kwa wahitimu wenye Diploma kupitia
Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana,”
Kwa maelezo
zaidi ya jinsi ya kuomba mafunzo kwa kutumia Mfumo wa Pamoja wa
Udahili (CAS), alisema Baraza linashauri waombaji watembelee tovuti ya Baraza ambayo ni www.nacte.go.tz.
No comments:
Post a Comment