Tuesday, March 01, 2016

BWENI LA WAVULANA WA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO.

 Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani. 
 Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa 3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka 2016.
Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu . 
 Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa nje kusbiri utaratibu mara baada waliofanikiwa kuokoa baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.

No comments:

Post a Comment