Thursday, March 10, 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. JOHN POMBE MAGUFULI, AMEMTEMBELEA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif aliruhusiwa kutoka hospitalini jana na hali yake inaendelea vizuri.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali  na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment