Mtangazaji kutoka kituo cha Radio cha Zenji FM Bw. Jumanne Ramadhani akifanya mahojiano na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis S.K Mutungi mara baada ya kufaya uangalizi katika kituo cha kupiga kura cha Nungwi kilichopo Unguja Zanzibar katika uchaguzi wa marudio.
Msajili wa Vyama vya Siasa akizungumza na mmoja wa wasimamizi wa Uchaguzi wa marudio mara baada ya kufika katika kituo cha kupiga kura cha Nungwi kilichopo Unguja Zanzibar katika uchaguzi wa marudio .
Wakazi wa Unguja na Pemba wametakiwa kuienzi Amani iliyopo Visiwani Zanzibar kwa kuachana na kufanya vitendo vinavyoweza kuleta uvunjifu wa Amani visiwani humu.
Rai hiyo imetolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi ambaye yuko visiwani humu akiwa na timu wa watu wanne kutoka ofisi yake kwa ajili ya uangalizi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika leo hii . Aliyasema hayo alipohojiwa na Mtangazaji wa kituo cha Radio cha Zenji Fm Bw.Jumanne Ramadhani mara baada ya kufanya uangalizi katika kituo cha kupiga kura cha Nungwi kilichopo Unguja Zanzibar. Ofisi ya Msajili ni miongoni mwa waangalizi wa ndani wa Uchaguzi waliofika Zanzibar kwa ajili ya uangalizi wa uchaguzi.
Aidha Jaji Mutungi ametoa rai kwa vyombo vya habari kuhakikisha vinalipoti masuala ya uchaguzi kwa ueledi ili visije vikawa chanzo cha uchochezi kwa jamii jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment