.RAIS JOHN MAGUFULI HII LEO AMEWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WAPYA ALIOWATEUA
HIVI KARIBUNI NA KUWATAKA WAKUU WA MIKOA HAO WAPYA KUHAKIKISHA VIJANA WANAFANYA
KAZI NA KUACHA UZEMBE.
. WIZARA YA NISHATI NA MADINI IMETOA TAMKO LA
SERIKALI LA UGUNDUZI MKUBWA WA GAS
KATIKA BONDE LA MTO RUVU MKOANI PWANI.
.WABUNGE NCHINI MYANMAR HII LEO WAMEMCHAGUA
MPAMBE WA KARIBU NA RAFIKI WA MUDA MREFU WA MPIGANIA DEMOKRASIA AUNG SAN SUU KYI KUWA RAIS WA KWANZA WA
KIRAIA NCHINI HUMO BAADA YA MIONGO MITANO.
.WAMAREKANI KATIKA MAJIMBO MATANO MAKUU
WANAJIANDAA KUPIGA KURA LEO KATIKA KILE KINACHOTARAJIWA KUWA KINYANG'ANYIRO
KIKUBWA CHA WAGOMBEA WA URAIS AMBAPO DONALD TRUMP ANALENGA KUIIMARISHA NAFASI
YAKE YA KUTAFUTA TIKETI YA REPUBLICAN.
HABARI KAMILI.
DAR ES SALAAM,
DAR ES SALAAM,
Rais John Magufuli hii leo amewaapisha wakuu wa
mikoa wapya aliowateua hivi karibuni na kuwataka wakuu wa mikoa hao wapya
kuhakikisha vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.
Rais Magufuli amewataka kuhakikisha kuwa hakuna
vijana watakaokwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao
wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.
Akizungumza kuhusu suala la wafanyakazi
hewa kwenye Halmashauri zote nchini Rais Magufuli
amesema amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa
kuhakikisha hakuna wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.
Wizara ya Mawasiliano,
Uchukuzi na Ujenzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA
imesema katika kuadhimisha siku ya Haki ya watumiaji wa mawasiliano Duniani
imewataka watumiaji wa mawasiliano kupeleka kero zao.
Akizunguma katika warsha
ya siku ya haki ya watumiaji wa mawasiliano Duniani Naibu katibu mkuu wizara ya
mawasiliano ,Uchukuzi na Ujenzi Dkt. Mary Sasabo amesema lengo la siku hiyo ni
kutoa elimu, kuandaa vipepelushi elekezi vya matumizi ya mawasiliano.
Kwaupande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Dkt. Ally Simba amesema wizi wa
simu za mkononi uko mbioni kufutika hapa nchini kutoka na kuwa simu yoyote
itakayo ibiwa itafungiwa haraka
Wizara ya nishati na
madini imetoa tamko la serikali la
ugunduzi mkubwa wa gas katika bonde la mto Ruvu mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es salaam Waziri wa Nishati na Madinip Prof.Sospeter
Mhongo amesema ugunduzi huo umefanywa na Kampuni ya Doxel na TPDC ambapo zaidi
ya futi za ujazo trilioni 2.17 wamegunduliwa katika eneo hilo.
Aidha ameongeza kuwa kituo
hicho kunaitwa MAMBA KOFI 1 na utafiti zaidi unaendelea ambapo hadi kufikia leo
Tanzania imegundua zaidi ya futi za ujazo trilioni 10.17 za nchi kavu na futi
za ujazo trilioni 47.08 za baharini jumla ikiwa ni trilioni 57.
NA HIZI NI HABARI ZA KIMATAIFA KUTOKA
WAPO REDIO FM.
Wabunge nchini myanmar hii
leo wamemchagua mpambe wa karibu na rafiki wa muda mrefu wa mpigania
demokrasia Aung San Suu Kyi kuwa rais wa kwanza wa kiraia nchini humo baada ya
miongo mitano.
Tin chau, mwenye umri wa
miaka 69, ameelezea kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo mkuu kuwa ni ushindi
wa suu kyi huku wabunge wakishangilia baada ya chau kutangazwa kuwa mshindi kwa
kupata kura 360 kati ya 652 zilizopigwa.
Rais huyo mpya ataapishwa
aprili mosi, kuchukua nafasi ya utawala wa miaka mitano wa rais anayeoondoka madarakani
Thein Sein aliyeungwa mkono na jeshi na kuliweka taifa hilo kwenye mkondo
sahihi wa kuondokana na utawala wa moja kwa moja wa kijeshi.
Wizara ya ulinzi ya urusi
imesema linaziandoa baadhi ya ndege zake za mizigo na kivita zilizoko katika
kituo cha jeshi la anga la urusi nchini syria na kuzirejesha nyumbani
kufuatia amri iliyotolewa na rais Vladmir Putin.
Taarifa hiyo ya wizara ya
ulinzi imekuja siku moja baada ya Putin kutangaza kuondoka kwa idadi kubwa ya
majeshi ya urusi nchini Syria, hatua ambayo inakwenda sanjari na kuanza kwa
mazungumzo ya amani ya Syria jijini Geneva.
Kuanza kwa mazungumzo hayo
hapo jana kulimpa Putin fursa nzuri ya kutangaza kumalizika kwa operesheni ya
urusi ya miezi mitano na nusu ya mashambulizi ya angani ambayo yameliwezesha
jeshi la syria kuyakomboa maeneo muhimu na kujiimarisha kabla ya mazungumzo ya
amani.
Rais wa Umoja wa Ulaya
Donald Tusk, leo anatarajiwa kuwa na mazungumzo nchini Cyprus na Uturuki kama
sehemu ya juhudi za kukamilisha masharti ya mpango wa Umoja wa Ulaya na Uturuki
wa kudhibiti mmiminiko wa wahamiaji barani Ulaya.
Habari zinasema rais huyo
wa Baraza la Ulaya, ambaye ataandaa mkutano mpya wa kilele kati ya Umoja wa
Ulaya na Uturuki, anakutana leo na Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades mjini
Nicosia na kusafiri kwenda Ankara kufanya mashauriano na Waziri Mkuu wa Uturuki
Ahmet Davutolu.
Uturuki na Umoja wa Ulaya
zimekubaliana kuhusu mpango mpya wa muda ili kujaribu kupunguza mmininiko wa
wakimbizi na wahamiaji Ulaya ambapo Umoja wa Ulaya umekubali kumpa makazi mapya
mkimbizi wa Syria kutoka katika kambi zilizoko Uturuki.
Wamarekani katika majimbo
matano makuu wanajiandaa kupiga kura leo katika kile kinachotarajiwa kuwa
kinyang'anyiro kikubwa cha wagombea wa urais ambapo Donald Trump analenga
kuiimarisha nafasi yake ya kutafuta tiketi ya Republican.
Katika siku iliyopewa
kichwa cha "Jumanne Kabambe ya pili" kinyang'anyiro cha uchaguzi wa
awali, kabla ya uchaguzi wa Novemba kitawapeleka wagombea wa Democratic na
Republican katika majimbo ya Florida, Illinois, Missouri, North Carolina na
Ohio.
Matokeo ya Florida,
Illinois na Ohio yatakuwa muhimu kwa vyama vyote viwili kutokana na idadi kubwa
ya wajumbe wanaopiga kura katika kila jimbo ambapo mgombea Wademocrat Hillary
Clinton anatarajiwa kuimarisha uongozi wake dhidi ya mpinzani wake Bernie
Sanders.
MWISHO WA TAARIFA YA HABARI KUTOKA WAPO RADIO
FM 98.1KWA TAARIFA NYINGINE YA HABARI UNGANA NASI SAA MOJA KAMILI JIONI.
No comments:
Post a Comment