Thursday, March 31, 2016

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAKABIDHI RIPOTI YA UTAFITI WA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA:


Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Casmir Kyuki akizungumza wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.
Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akizungumza wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma. Makabidhiano yalifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria Dar es Salaam.

WABUNGE WATATU WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha Mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a). Wabunge hao ni Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero ; Mheshimiwa Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibala.

Wabunge hao wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mh.Thomas Simba. Akisoma mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiwa wote watatu waliomba rushwa ya shilingi Mil.30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo kwa lengo la kumsaidia ili Taarifa ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa kwa wakati huo ijadiliwe tahere 16/3/2016 ipitishwe bila marekebisho.

Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na washtakiwa wote watatu mahakama imewaachia kwa dhamana ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 5. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 14/4/ 2016 itakapotajwa tena. 

TAKUKURU inawajulisha wananchi wote kwamba hakuna mtu ambaye yupo juu ya Sheria. Rushwa haivumiliki!


IMETOLEWA NA 
OFISI YA AFISA UHUSIANO 
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU 
31 MACHI, 2016

Wednesday, March 30, 2016

CHUO CHA UTALII KUANZA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA.

CHUO cha utalii chenye kampasi tatu ambazo ni Kampasi ya Bustani, Kamapasi ya Temeke na Kampasi ya Arusha wameanza kudahili (kuandikisha) wanafunzi wapya kwa 2016/2017.

Afisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma wenye sifa za kusoma chuo hicho amewaomba watembelee tovuti ya Baraza la ufundi la Taifa (NACTE) www.nacte.go.tz
Afisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusina na chuo hicho kuwa na kozi tofauti tofauti zinazoweza kuwasaidi wananchi na hata kujiali weyewe kutokana na mafunmzo yanayotolewa katika chuo hicho. Kulia ni Meneja wa chuo cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam, Steven Madenge.
Meneja wa chuo cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam, Steven Madenge akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. kushoto ni fisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma.
Mkurugenzi wa Mfumo wa shughuli za kitaalam wa chuo cha Utalii, Naiman Mbise akifafanua jambo mbele ya waadnishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Afisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kutoka kushoto ni Msajili wa chuo cha utalii, Ishaka Perpetua, Mkurugenzi wa Mfumo wa shughuli za kitaalam wa chuo cha Utalii, Naiman Mbise na Kulia ni Meneja wa chuo cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam, Steven Madenge.

MWANZA NA ARUSHA YAONGOZA WATUMISHI HEWA.

 Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik  akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 116.4 KUTOKA JAPAN.

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano walizosaini na Serikali ya Japan utakaoitakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
 Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.(Na Eleuteri Mangi-MAELEZO).

 Na Eleuteri Mangi-MAELEZO


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.


Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili  unahusu masuala ya kiufundi  yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa  Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini. 
Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.
Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji  kuwekeza nchini Tanzania.

Adha amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500. 

JAJI MKUU WA TANZANIA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MAHAKAMA KATIKA MIKOA YA IRINGA, NJOMBE NA RUVUMA, AISIFU MAHAKAMA KANDA YA SONGEA KWA KUFANYA VIZURI.

Mahakama ya Tanzania ni moja kati ya Taasisi iliyopo katika mchakato wa kuboresha huduma zake. Katika kufanikisha azma hii jitihada/maboresho mbalimbali yameendelea kufanyika ili kuwezesha Mhimili huu muhimu kuwa na mazingira rafiki ya utoaji haki kwa wananchi.


Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alitembelea katika Mahakama za mikoa ya Iringa, Njombe pamoja na Ruvuma, lengo la ziara ikiwa ni kukagua na kujionea hali ya utendaji wa Mahakama na mwenendo wa uendeshaji wa mashauri.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Songea.
 
Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu alipata nafasi ya kutembelea Mahakama Kuu Songea, Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mahakama ya Wilaya Songea. Mahakama ya Wilaya Mbinga, Mahakama ya Wilaya Nyasa inayotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni na baadhi ya Mahakama za Mwanzo.

Mhe. Jaji Mkuu aliongozana na Watendaji wengine wa Mahakama katika ziara yake ambao ni; Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Msajili Mkuu pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Wote walipata fursa ya kujionea hali halisi ya miundo mbinu ya Mahakama ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za Mahakama hizo kutoka kwa Jaji Mfawidhi/Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hizo. 
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa kwanza kushoto) akipata taarifa fupi ya Mahakama Kanda ya Songea kutoka kwa Mhe. John S.Mgetta, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea (aliyesimama), mara baada ya kuwasili Mahakama Kuu kanda ya Songea.

Akisoma taarifa yake mbele ya Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. John Mgetta, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Songea alisema kuwa Kanda yake ina Mahakama Kuu moja (1), Mahakama ya Hakimu moja (1) ya Mahahakama za Wilaya tano (5) ambazo ni Songea, Namtumbo, Tunduru, Mbinga na Mahakama ya Wilaya Nyasa.

Hata hivyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. John Mgetta alikiri Mahakama yake kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi hususani Makarani na ubovu wa majengo ya Mahakama, kwani hayatoshi na ni machakavu.

Mhe. Jaji Mkuu, Kanda ya Songea inakabiliwa na uhaba wa watumishi, hususani makarani. Ukiachia mbali changamoto hii tunakabiliwa pia na uchakavu wa miundombinu ya majengo.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (kushoto), Mhe. John S.Mgetta Jaji Mfawidhi Kanda ya Songea (kulia), wakisoma majalada ya kesi katika Mahakama ya Mwanzo Kigonsera mkoani Songea.

 “Mhe. Jaji Mkuu, majengo mengi yanayotumiwa na baadhi ya Mahakama mfano Mahakama Hakimu Mkazi na Wilaya za Songea pamoja na Mahakama nyingi za Mwanzo ni ya kuazima. kwa ujumla hali ya majengo ya Mahakama katika Kanda hii si ya kuridhisha, Mahakama nyingi zina majengo mabovu sana, hasa Mahakama za Mwanzo, ama yanahitaji ukarabati mkubwa au kubomolewa na kujengwa upya,” alieleza Mhe. Jaji Mgetta.

Licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa, Mahakama Kanda ya Songea ni moja ya Kanda inayoongoza nchini kwa umalizaji wa Mashauri yanayofunguliwa katika Mahakama mkoani humo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Tehama, Mahakama ya Tanzania, Bw. Machumu Essaba alisema kwa mujibu wa Takwimu za uondoshaji wa Mashauri nchini, Kanda ya Songea ndio inayoongoza kwa kasi kubwa ya kumaliza kwa wakati kesi zinazofunguliwa.

“Napenda nikiri kuwa Kanda ya Songea ndio Kanda inayoongoza kwa uondoshaji wa Mashauri, hii inatokana na jitihada zifanywazo na Majaji na Mahakimu wa Mahakama katika kanda hiyo,” alisema Essaba.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Songea ina jumla ya Majaji wawili tu na kuongeza kuwa kila Jaji anawastani wa mzigo wa kazi (work load) wa kesi 215 kwa kila mmoja. 

Alisema; uwezo wao wa kumaliza mashauri yanayofunguliwa (clearance rate) ni 154% na kila kesi iliyofunguliwa ilimalizika kwa wakati kwa asilimia 100% huku wakiendelea kutoa maamuzi ya kesi za zamani kwa asilimia 54%.
Kwa upande wa Mahakama ya Mkoa/Hakimu Mkazi, Mkurugenzi Msaidizi huyo alisema Mahakama hiyo haina kesi yenye Zaidi ya miezi 18 Mahakamani na kuongeza kuwa Mahakama hiyo ina jumla ya Mahakimu wanne (4) wenye wastani wa mzigo wa kazi wa kesi 117 na uwezo wao wa kuondoa mashauri yanayoingia ni asilimia 112, na kuongeza kuwa utendaji huu unarudisha Imani ya Mahakama kwa wananchi.

Bw. Essaba aliendelea kueleza juu ya utendaji wa Mahakama katika Kanda ya Songea, kwa kuongeza kuwa kuna jumla ya Mahakama za Wilaya nne (4) Mahakama zote zikiwa na jumla ya Mahakimu sita (6) na kila mmoja ana wastani wa mzigo wa kazi ‘workload’ wa kesi 186 na uwezo wao wa kuondoa kesi zinazofunguliwa ni asilimia 135 na kupelekea kumaliza mlundikano wa mashauri katika Mahakama hizo.

Bw. Essaba alimaliza kwa kuongelea juu ya Mahakama za Mwanzo zilizopo Kanda ya Songea ambazo jumla yake ni 45 na kuongeza kuwa Mahakama hizo zina jumla ya Mahakimu 52 ambapo kila mmoja ana mzigo wa kazi wa kesi 157 na uwezo wao wa kuondoa kesi zinazofunguliwa kwa Mahakama zote za Mwanzo ni 104.

“Hakuna kesi/shauri lolote lililokaa kwenye Mahakama hizo zaidi ya mwaka mmoja, kwa ujumla Kanda ya Songea ni moja ya kielelezo cha utendaji uliotukuka katika Mahakama ya Tanzania,” alisisitiza Essaba.

Hata hivyo; Mahakama ya Tanzania kwa ujumla wake ipo katika mchakato wa maboresho, ulioanza muda wa takribani miaka mitatu sasa wa kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuondosha mashauri ya muda mrefu Mahakama na kutoruhusu Mashauri kukaa Mahakamani Zaidi ya miaka miwili (2).

Kwa upande wake Mhe. Jaji Mkuu, aliupongeza uongozi wa Mahakama Kanda ya Songea kwa jitihada zao za dhati katika kuhakikisha wanatoa haki kwa wakati, na kuongeza kuwa hali hii inawapa Imani wananchi na kuifanya Mahakama kuwa kimbilio lao katika upatikanaji wa haki.
Kwa upande wao Watendaji walioambatana na Mhe. Jaji Mkuu katika ziara yake walisema wamefarijika sana na kasi ya Kanda ya Songea kwa uondoshaji wa Mashauri na kudai kuwa hali hii imesababisha hata idadi ya wafungwa/mahabusu gerezani kupungua.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati, akipitia jalada moja baada ya jingine kuona hali halisi ya utoaji haki kwa Wananchi katika Mahakama ya Mwanzo Kigonsera mkoani Songea.
“Binafsi nimefarijika sana na mabadiliko tuliyoyaona Songea, idadi yawafungwa imepungua ghafla na wananchi walio wengi wanaonekana kufurahia na kusifu jitihada hizi za Mahakama mkoani Ruvuma,” alisema Mhe. Katarina Revokati, Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania.
Pamoja na jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanyika kuboresha huduma za Mahakama nchini, Mhe. Jaji Mkuu aliwasihi watumishi kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi na kanuni zilizowekwa.
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, (katikati), Mhe. John Mgetta, Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu Kanda ya Songea (wa pili kushoto), Mhe. Salima Chikoyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kushoto), Mhe. Katarina Revocati, Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu wa Mkoa wa Songea.

WATAALAMU WA MOYO KUJADILI JINSI YA KUKABILI, APRILI 21 NA 22 KATIKA UKUMBI WA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR.

 Mwenyekiti wa Madaktari bingwa wa  ugonjwa wa Moyo, Robart Mvungi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusia na  mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Aprili 21 na 22 mwaka huu, Amesema kuwa Mkutano huo utakuwa kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa wa Moyo ambao sio wa kuambukizwa. 

Pia amesema kuwa mkutano huo utahudhuliwa na Madaktari bingwa ugonjwa wa moyo  pia watatumia muda huo kuelimisha jamii ili kuweza kupunguza ongezeko la ugonjwa wa moyo hapa nchini.
Kushoto ni Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete, Ruben Muta, Mwaandaaji wa mkutano, Adeline Ndesanja na Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete,Tulizo Sanga.
 Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete,Tulizo Sanga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari( hawapo pichani) jijini Dar es Salaam .

Tuesday, March 29, 2016

TAMASHA LA PASAKA LAHITIMISHWA MJINI KAHAMA MKOA WA SHINYANGA:

23
Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisoma hotuba kwa niaba ya waziri Profesa Mbarawa katika tamasha hilo kushoto ni Alex Msama wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa na Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba.24
Mwimbaji Upendo Nkone akiwaimbisha mashabiki wake wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
kwaani huku mashabiki wakicheza kwa furaha.
18
Mashabiki wakicheza kwa furaha katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.

Monday, March 28, 2016

WAFANYABIASHARA WA MAFUTA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI WA BOMBA LA MAFUTA LINALOGHRAIMU DOLA BILIONI NNE.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Bomba la Gesi litakalokuwa likisafirisha kutoka Tanga kwenda uganda. 
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wa mafuta nchini(NICOL), Gidion Kaunda akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya Katibu mkuu kuzungumzia bomba la mafuta la Tanga kwenda Uganda.

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO ANASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA KITUO CHA UTAMADUNI KILICHOPO CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA:


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akiwaangalia wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha (hawapo pichani) wakicheza ngoma ya kabila la wa Meru wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo. Kulia ni Randall Stubbs ambaye ni Meneja Mradi wa kituo hicho kinachojengwa chuoni hapo, watatu kulia ni Afisa Michezo wa Mkoa Mwamvita Okeng’o na wa nne kulia ni Afisa utamaduni wilaya ya Arumeru Senyael Pallangyo.

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA MKUU WA MKOA MPYA WA SONGWE MHE. CHIKU GALLAWA IKULU DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam  Machi 28, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshuhudia Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akiweka sahihi katika hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam  Machi 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini hati ya kiapo cha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam Machi 28, 2016

RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI KUTOKA KWA MKAGUZI NA MDHIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) IKULU DAR ES SALAAM :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam  Machi 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiwa na watendaji wakuu  wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkafuzi Mkuu wa hesabu za serikali  baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam Machi 28, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakipitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali iliyokabidhiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam  Machi 28, 2016.PICHA NA IKUL

AJALI YA BASI LA LUPONDIJE EXPRESS KUTOKA MWANZA - IRINGA LAUA WATANO USIKU MKOANI IRINGA , DEREVA AKIMBIA:

 Askari   polisi na  wasamaria  wema  wakisaidia  kutoa maiti  kutoka katika  basi la Lupondije Express namba T 798 AKV kutoka Mwanza - Iringa baada ya  kupinduka  eneo la Mteremko wa Ipogolo mjini Iringa usiku  wa  leo 
 Gari la kikosi  cha  Zimamoto na uokoaji  likiwa  eneo la  tukio  kusaidia  kuokoa maisha ya majeruhi 

YEYOTE ATAKAYE KIMBILIA KWENYE VYOMBO VYA DOLA KULISHITAKI KANISA ATAONA CHA MOTO:


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema mkoa wake hauko salama kama watu wanavyodhani kwa sababu silaha nyingi zinamilikiwa kiholela na mafunzo ya matumizi ya silaha hizo hutolewa hata kwa watoto.

Makonda alisema hayo wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kuhakiki silaha zao na kusalimisha zile zinazomilikiwa kinyume cha sheria.

Alisisitiza kwamba ifikapo Julai Mosi, operesheni maalumu ya kukamata silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria itaanza na yeye mwenyewe ndiye atakayeiongoza.

“Tumegundua kwamba kwenye bonde la mto unaotenganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, kuna mafunzo yanatolewa kwa watoto. Wazazi wanadhani watoto wao wamekwenda shule  kumbe wamechukuliwa huko.Hatuwezi kukubali hali hiyo iendelee."Alisema

SOMO: ROHO MTAKATIFU NA KARAMA ZAKE (3)

Askofu Sylvester Gamanywa, Mwangalizi Mkuu WAPO MIssion International. 
Wiki iliyopita tulifanya  uchambuzi wa fungu la karama za NGUVU ambazo ni karama ya Imani, Matendo ya miujiza na karama za kuponya magonjwa. Leo tunahitimisha kipengele hiki kwa kuchambua fungu la mwisho la karama za MAWASILIANO ambazo ni karama ya unabii, aina za lugha na tafsiri za lugha:
Tafsiri ya Karama ya unabii

Fungu la karama za mawasiliano ambazo ni “karama ya unabii”; “karama ya aina za lugha” na “karama ya tafsiri za lugha” Nitaanza na “karama ya unabii.” Kwanza kabla ya kutafsi karama tuanze na msamiati wa neno “unabii” kwa mujibu wa Biblia.  “unabii” ni ujumbe maalum kutoka kwa Mungu, ukiletwa na Roho Mtakatifu na kufunuliwa kwa mpokeaji/nabii/mtu aliyeteuliwa kwa wakati huo kuuwasilisha ujumbe huo kwa walengwa.

Ujumbe huu wa kinabii unapotangazwa na msemaji aliyeupokea, lazima uwasilishwe kwa lugha inayojulikana na wasikilizaji. Lazima ujumbe huo uwe umebeba taarifa ambazo mlengwa akiusikia atajitambua kuwa ujumbe huo ni wa kwakwe. Kwa maelezo mengine, unabii ni ujumbe wa Mungu kupitia kwa mpokeaji ili auwasilishe kwa walengwa pasipo yeye kuingiza mawazo yake ya kibinandamu.

Sasa tuje kwenye tafsiri ya “karama ya unabii”. Tafsiri nyepesi kueleweka kwa wazi zaidi ni “mpokeaji kupokea “zawadi ya kutumika kuwasilisha ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kuwajenga, kuwafariji na kuwatia moyo walengwa wa unabii huo; “Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, kuwafariji, na kuwatia moyo.” (1 Kor.14:3)

Sunday, March 27, 2016

RAIS MAGUFULI AITAKIA HERI TAIFA STARS

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NEMBO YA TAIFATAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitakia heri timu ya Taifaya Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wake dhidi ya Timu ya Taifaya Chad,utakaofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam,kesho tarehe 28 Machi, 2016.
Taifa Stars itacheza mchezo huo wamarudiano,ikiwani wiki moja tangu ilipocheza mchezo wa kwanza,katika Jiji la N’Djamena nchini Chad ambapoTaifa Stars ilishindabao 1 – 0.
Katika salamu hizo Rais Magufuli amewataka wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF),kutambua kuwa watanzania wanamatumaini makubwa kuwa timu yaoi tafanya vizuri katika mchezo huo,ikiwa nijuhudi za kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la soka barani Afrika,zitakazofanyika Gabon hapo Mwaka ujao wa 2017.
“Watanzania wote tuiombee timu yetu ifanye vizuri, ushindi wa Taifa Stars niheshima kwa nchi yetu na sifa muhimu kimataifa, mimi naamini kama tulishinda N’Djamena tunao uwezo wakushinda hapokesho”amesisitizaRaisMagufuli
Gerson Msigwa
KaimuMkurugenziwaMawasiliano, IKULU
Dar essalaam
27 Machi, 2016

MLINZI WA NYUMBA YA KULALA WAGENI MAENEO YA CHALIZE MKOANI PWANI AWAJERUHI MADEREVA WATATU WA MAGARI MAKUBWA:


Madereva watatu wa malori yaendayo mikoani na wasaidizi wao watatu, wamenusurika kifo baada ya kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwilini na mlinzi wa nyumba moja ya wageni iliyopo Ubena, Chalinze mkoani Pwani.

Tukio hilo limetokea jana alfajiri saa 11.30 kwenye hoteli hiyo ambako madereva na wasaidizi hao walikuwa wamefikia kwa mapumziko kabla ya kuendelea na safari. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventura Mushongi alisema tukio hilo lilitokea baada ya kuwapo kutokuelewana kati ya mmoja wa madereva na mlinzi wa nyumba hiyo.

Kamanda Mushongi alisema taarifa za awali zinasema baada ya mabishano hayo ambayo bado hayajajulikana chanzo chake, mlinzi huyo alikoki silaha yake aina ya Shortgun na kupiga risasi moja hewani kutuliza vurugu na kumjeruhi mmoja wa madereva hao.

Hata hivyo, mabishano yalizidi baada ya madereva wengine kujitokeza kuingilia ndipo mlinzi huyo akapiga risasi nyingine ambayo ilitoka na gololi zake kusambaa na kuwajeruhi wengine wanne ambao walipelekwa Kituo cha Afya Chalinze kwa matibabu.

Alisema mlinzi huyo amekimbia na anaendelea kutafutwa na chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Chalinze, Dk Victor Bamba alisema walipokea majeruhi watano ambao walipatiwa huduma ya kwanza na kutokana na hali zao kuwa mbaya walihamishiwa Hospitali ya Tumbi.

Akizungumza wodini Tumbi walikolazwa, mmoja wa madereva hao, Harun Adeli alisema walifika hapo juzi saa mbili usiku na kuamua kulala ndani ya magari yao ili jana waendelee na safari na ilipofika saa kumi na moja alfajiri walisikia makelele yanayoashiria ugomvi ndani ya hoteli hiyo.

“Wakati tunashangaa tulishtukia risasi zinarindima na ndipo zilipotufikia,” alisema.

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Tumbi, Habibu Yahaya alisema aliwapokea majeruhi Stephen Fredy, Beno Henry, Akrey Dallu, Ramadhani Saidi, Amani Almasi na Adel wote wakazi wa Dar es Salaam.

Diwani wa Ubena, Nicolaus Muyunga alisema kwa mujibu wa majirani, yalitokea mabishano kati ya utingo na dereva ambao walikuwa wamekunywa na kulala kwenye meza muda mrefu, walipotakiwa kuchukua vyumba wakalale ndani au warudi katika magari yao walikataa na mlinzi alipotaka kuwaondoa kwa nguvu walimzidi nguvu, hivyo akajitetea kwa kupiga risasi hewani.;