Showing posts with label Askofu Valentino Mokiwa. Show all posts
Showing posts with label Askofu Valentino Mokiwa. Show all posts

Monday, March 28, 2016

YEYOTE ATAKAYE KIMBILIA KWENYE VYOMBO VYA DOLA KULISHITAKI KANISA ATAONA CHA MOTO:


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema mkoa wake hauko salama kama watu wanavyodhani kwa sababu silaha nyingi zinamilikiwa kiholela na mafunzo ya matumizi ya silaha hizo hutolewa hata kwa watoto.

Makonda alisema hayo wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kuhakiki silaha zao na kusalimisha zile zinazomilikiwa kinyume cha sheria.

Alisisitiza kwamba ifikapo Julai Mosi, operesheni maalumu ya kukamata silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria itaanza na yeye mwenyewe ndiye atakayeiongoza.

“Tumegundua kwamba kwenye bonde la mto unaotenganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, kuna mafunzo yanatolewa kwa watoto. Wazazi wanadhani watoto wao wamekwenda shule  kumbe wamechukuliwa huko.Hatuwezi kukubali hali hiyo iendelee."Alisema