Naibu Waziri wa Afya. Dk.Kigwangalla akiwa katika vipumo hivyo..
Naibu
Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akiwa katika kupima macho kwenye kambi maalum ya
kutoa huduma za matibabu ya bure yaliyoandaliwa na Care Foundation na wadau
wengine katika viwanja vya Bustani ya Jiji, Posta Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla
ahimiza Jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya zao.
Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla
amehimiza Jamii kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara katika hali ya
kubaini matatizo yanayowakabili ilikuchukua hatua ikiwemo kupata tiba mapema.
Dk.
Kigwangalla ametoa kauli hiyo mapema leo Februari 28.2016, jijini Dar es
Salaam, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kambi maalum ya kupima afya bure
kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Ilala kwa kuandaliwa na Care
Foundation na wadau wengine wa afya ikiwemo Hospitali ya Ebrahim Haji Chartable
Health Centre ambao wanasimamia kutoa huduma za matibabu kwa kushirikiana na
taasisi zingine.
Akitoa hutuba
yake fupi, kwa wananchi mbalimbali walifika katika tukio hilo la kupatiwa
matibabu hayo ya bure, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla amesema Jamii wanatakiwa
kuwa na maisha yenye afya hivyo zoezi la kupima afya mara kwa mara ni bora
zaidi kaika kuimalisha afya ya mwili.
“Wananchi
wapo na wakati mwingi wakifanya shughuli zingine na hata muda kupima afya
inakuwa ngumu. Kukinga ni bora Zaidi kuliko tiba. Zoezi hili litasaidia sana
wananchi wengi na tunaomba muendelee na maeneo yote ya nchi yetu.” Ameeleza
Dk.Kigwangalla.
Aidha, Dk.
Kigwangalla amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Hazan Zungu kwa
kuwezesha kuandaa zoezi hilo kwa kushirikiana na wadau hao kwani ni mfano bora
wa kuigwa na wabunge wengine pindi wapatapo nafasi ya kutumikia jamii
iliyowachagua.
Pia katika
zoezi hilo, Mbune wa jimbo la Ilala, Mh. Mussa Zungu na Naibu Waziri Dk.
Kigwangalla walipata wasaha wa kupima afya zao pamoja na kutembelea maeneo ya
kutolea huduma na kushuhudia namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi.
Kambi hiyo ya
matibabu, inatoa matibabu hayo bure kwa wananchi wote wanaofika hapo ambapo pia
mbali na matibabu wanatoa huduma ya dawa huku wakitoa pia mawani kwa watu wenye
matatizo ya macho.
Watu mbalimbali wamekaribishwa kupatiwa matibabu hayo ambayo
pia yanatolewa na madaktari bingwa wa magonjwa husika.
No comments:
Post a Comment