Monday, July 10, 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA KITUO CHA AFYA CHA KATORO NA KUJIONEA HALI YA KITUO HICHO

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa kitupo cha afya cha mji mdogo wa Katoro.Waziri huyo amefika katika  kituo hicho ili kujionea hali ya kituo hicho ambacho kinahudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huo pamoja na jirani zake licha ya kuwa na changamoto ya watumishi pamoja na miundombinu

Waziri Ummy akimsalimia mtoto aliyefika kituoni hapo pamoja na mama yake kupata huduma ya afya,kulia ni Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dkt. Peter Janga
Moja ya Vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano ni Upatikanaji wa Dawa kwenye vituo vyote vya Serikali,Waziri Ummy Mwalimu akiongea na watoa huduma kwenye dirisha la dawa katika kituo hicho.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akimfafanulia jambo mmoja wa wagonjwa waliofika kupata huduma kwenye kituo cha afya cha Katoro

Waziri Ummy akitoa maelekezo kwenye matangazo yaliyobandikwa kwenye kuta za kituo hicho,kushoto ni Mkurugenzi wa HALMASHAURI YA Geita Lawrence Kalabezile.Waziri huyo amewataka watumishi wa kituo hicho kujituma na kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wananchi hususan katika kuokoa maisha ya wagonjwa.

\
Katika ziara hivyo Waziri Ummy alikagua ujenzi wa jengo la upasuaji wa dharura unaojengwa kwenye kituo hicho.Waziri wa Afya yupo  katika ziara ya kikazi ya  siku tatu Mkoani Geita (PICHA ZOTE NA WIZARA YA AFYA)



No comments:

Post a Comment