Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt
Hamis Kigwangalla kwa mara ya kwanza ametoa sababu ya yeye kushindwa
kuweka wazi orodha ya watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja
(mashoga).
Amesema hakuweza kuyataja hadharani majina hayo kwa kuwa alisikiliza ushauri aliopewa na jamii inayomzunguka.
“Mimi
nashaurika, sikuweka majina hadharani kwa sababu nashaurika, listi ya
watu ninayo na tunachukuwa hatua kimya kimya hili ni kosa la jinai na
mtu anayekutwa na hatia anafungwa kifungo cha miaka 30 jela” Amesema Dkt. Kigwangalla
Dkt.
Hamisi Kigwangalla amesema, hayo wakati akiwa kwenye maadhimisho ya
siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es
Salaam.
Katika
maadhimisho hayo Kigwangalla ameeleza kuwa kufanya mapenzi ya jinsia
moja ni kosa kibaiolojia na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia
yake.
Aidha,
amesema katika sheria iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya
mapenzi ya jinsia moja, kuna kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua
endapo ikithibitika amekaa mapozi yasiyoeleweka na ikabainika kuwa ni
kwa lengo la mapenzi ya jinsia moja atafunguliwa mashtaka.
Mhe.
Kigwangalla amewaonya wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na
kusisitiza kwamba serikali inawachukulia hatua kimya kimya.
No comments:
Post a Comment