Monday, April 04, 2016

WAHAMIAJI WAANZA KUFURUSHWA UGIRIKI:

Uturuki

Image copyrightAP
Image captionUturuki inatarajia kupokea wahamiaji 500

Maboti ya kwanza yaliyowabeba wahamiaji ambao wanafurushwa kutoka Ugiriki na kupelekwa Uturuki yameanza safari chini ya mpango wa EU unaotarajiwa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Mamia ya wahamiaji wameonekana wakiabiri feri katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki mapema Jumatatu.
Wanapelekwa Dikili, magharibi mwa Uturuki.
Maafisa wa Uturuki wamesema wanatarajia kupokea karibu watu 500.
Mkataba kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki umeshutumiwa vikali na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na kuna wasiwasi pia kuhusu maandalizi duni.
Wahamiaji nchini Ugiriki wamelalamika kwamba hawana habari za kutosha kuhusu utaratibu wa kuomba hifadhi na wengine wamesema hawafahamu kwamba wanaweza kurejeshwa Uturuki.
Idara ya EU inayohusika na kuwasindikiza watu na kuwavusha bahari ya Aegean ina chini ya asilimia kumi ya wafanyakazi inaohitaji kutekeleza jukumu hilo, shirika la habari la Associated Press limeripoti.
Feri nyingine inayobeba wahamiaji kuwapeleka Uturuki inatarajiwa kuondoka kisiwa cha Chios nchini Ugiriki baadaye Jumatatu.

MkatabaImage copyrightAFP
Image captionWahamiaji wamekuwa wakipinga mkataba huo

Chini ya mkataba huo wa EU, wahamiaji wanaowasili kwa njia haramu Ugiriki wanatarajiwa kurejeshwa Uturuki wasipowasilisha maombi ya kutafuta hifadhi au maombi yao yakikataliwa.
Kwa kila mhamiaji wa Syria anayerejeshwa Uturuki, EU inapangiwa kumpokea mhamiaji mwengine wa Sryia ambaye ombi lake limekubaliwa.
Uturuki itanufaika kifedha na kisiasa kutoka kwa umoja huo chini ya mkataba huo.
Tangu kutiwa saini kwa mkataba huo mwezi Machi karibu watu 400 wamekuwa wakiwasili kila siku visiwa vya Ugiriki.
Wahamiaji milioni moja waliingia Ulaya kupitia Ugiriki kwa kutumia maboti kutoka Uturuki mwaka jana.
Source BBC

No comments:

Post a Comment