Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya
sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu
ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu
wakati wanafunzi wakiwa madarasani.
Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini
Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme
majira saa 3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na
ajali hiyo ya moto.