Friday, March 04, 2016

NACTE YAUZINDUZI WA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CENTRAL ADMISSION SYSTEM (CAS)) KWA MAFUNZO YANAYORATIBIWA NA BARAZA KWA MWAKA WA MASOMO WA 2016/17.

Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na Uzinduzi  wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)    wapili kushoto ni   Mkuu wa Kitengo cha Udahili Seremani Majindo, Mkurugenzi wa Mfumo na Upimaji,Bakari Issa  na  Kaimu Mkurugenzi Idara ya vyuo na ushauri na Mipango.Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam 

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limetangaza ufunguzi rasmi wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree”).

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maelekezo na Msaada kwa Taasisi wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga amesema kuwa, kwa mwaka wa masomo wa 2015/16, Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za astashahada (Cheti) na stashahada (Diploma) kwa mafunzo ya afya na ualimu yaliyoidhinishwa na Baraza. ameongeza kuwa, Baraza pia  lilishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)).

“Mifumo hii miwili ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha  waombaji kudahiliwa. Mifumo hii ya udahili imekuwa na mafanikio yafuatayo: Kudhibiti udanganyifu katika udahili uliotokana na baadhi ya waombaji kutumia vyeti vya bandia, kuwapunguzia waombaji gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mwombaji udahili mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja na kuwanyima waombaji wengine nafasi, kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji udahili kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini, na kuwawezesha waombaji udahili kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali,” alieleza.

Dk Rutayuga alieleza kuwa, kwa kutambua mafanikio ya udahili wa pamoja  yaliyopatikana,  Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeamua kuwa maombi yote ya udahili kwa ajili ya mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) yafanywe kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS). 

Amefafanua kwamba. Baraza linautangazia umma kuwa, kuanzia mwaka wa masomo 2016/2017 udahili wa kozi zote nchini utafanywa kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaosimamiwa na NACTE, Vyuo Vikuu  na taasisi za Elimu zote nchini Tanzania zinazotoa mafunzo ya Cheti na Diploma kutodahili wanafunzi nje ya mfumo wa udahili wa Pamoja kuanzia mwaka wa masomo 2016/17.

“Tunapenda kutoa taarifa pia kuwa, maombi ya kujiunga na kozi za Cheti na Diploma yataanza kupokelewa rasmi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana. Baraza pia litaanza kupokea rasmi maombi ya kujiunga na kozi za Shahada (Degree) kwa wahitimu wenye Diploma kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana,” 

Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuomba mafunzo kwa kutumia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS), alisema Baraza linashauri waombaji watembelee tovuti ya Baraza ambayo ni www.nacte.go.tz.

Tuesday, March 01, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, DKT. HAMISI KIGWANGALLA AMEAGIZA KUFUNGWA KWA DUKA LA DAWA ZA BINADAMU LA SHINE CARE PHARMACY LILOPO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo kinyume na sheria.

Mmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.

BWENI LA WAVULANA WA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO.

 Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani. 
 Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa 3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. 

UKWELI KUWA OLDUVAI GORGE IPO MKANI MANYARA NA SIO KENYA.

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTubehttps://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.

Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.

SHILINGI LAKI MOJA YAMPONZA DAKTARI WA HOSPITALI YA LIGULA AMBAYO NI YA MKOA WA MTWARA.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.

·         Ni baada ya kudai rushwa ya sh. 100,000/- kumfanyia upasuaji mgonjwa.
·         Mama alilazimika kuuza shamba ili apate fedha za kumtibia baba yake
·         Aagiza maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo yafungwe leo hii
·         Amwagiza RAS aitishe kikao cha watumishi wote leo saa 9 alasiri
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-.

Monday, February 29, 2016

NEEMA YAWAANGUKIA WALIMU WA SERIKALI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM KUSAFIRI BURE KWA DALADALA

 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini.
 Mwenyekiti wa Chama Chama Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es salaam, Said Mabrouk(wa kwanza kushoto) akizungumzia mwitikio wa wamiliki hao kuhusu kuwasafirisha walimu ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Konondoni Mh. Paul makonda na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kutoa elimu bure hapa nchini, kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Madereva, Shabani Mdemu, wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William Masanja.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William Masanja akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sunday, February 28, 2016

MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI TANGA KWA ZIARA YA SIKU MBILI ZA KIKAZI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantum Mahiza alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku Mbili Mkoani humo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.(Picha na OMR).