Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es salaam wakati
alipozungumzia mpango wa kuwasafirishwa walimu bure jijini Dar es salaam wakati
wa kwenda na kurudi kazini huku akiwa ameongozana na viongozi wa vyama vya
usafirishaji wa abiria jijini Dar es salaam pamoja na viongozi wa Madereva wa
Daladala jijini Dar es salaam.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Na Chalila
Kibuda, Globu ya Jamii.
WALIMU wa
Shule ya Msingi na Sekondari Mkoa wa Dar es Salaam watasafiri na Daladala bure
kuanzia Machi 7 mwaka huu.
Akizungumza
na waadishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda amesema kuwa kutokana na changamoto za walimu ameona kuna umuhimu wao
kusafiri bure waweze kupunguza makali ya nauli za kila siku wanapopanda
daladala hizo.
Amesema kuwa
walimu watasafiri kwa usafiri huo kuanzia saa 11:30 hadi saa 2 kwa muda
wa asubuhi na baada ya muda huo kupita watalipa nauli zao na nyakati za jioni
watarudi majumbani mwao kwa kupanda daladala hizo kuanzia saa 9 hadi saa
12.Makonda amesema kuanzia kesho watatengeneza vitambulisho vya walimu wote wa
serikali wa mkoa wa Dar es Salaam ambavyo wataonyesha kwa makondakta wa
daladala vikiwa na saini ya mkuu mkuu wa Wilaya.
Amesema
utaratibu huo utakuwa ukitumika kwa siku za kazi tu kwa walimu kupanda bure na
sio vinginevyo na walimu wanaoishi mikoa mingine na wanafundisha Dar es Salaam
watalipa nauli zao kufika katika vituo vyao vya kazi.
Aidha amesema
kuwa walimu wataingia katika Daladala wasiopungua wawili na wengine watasubiri
daladala zingingine kutokana na maoni ya wamliki wa vyombo vya usafiri.Nae
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam, Sabri
Mabroock amesema kuwa wanaunga mkono sera ya elimu ya Rais Dk.John
Pombe Magufuli.
Amesema
walimu wamekuwa na changamoto wakati mwingine wanashindwa kulipa hata nauli
hivyo kupanda bure watakuwa wamerahisisha maisha.
No comments:
Post a Comment