Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akizungumza machache na wananchi waliofika katika uzinduzi huo.
Friday, December 15, 2017
Friday, November 03, 2017
DC KIBAHA AUAGIZA UONGOZI WA KAMPUNI YA YAPI MARKEZI KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI
Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Asumpter Mshama akimtambulisha meneja mwajiri wa kampuni ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Yapi Markezi kutoka Uturuki kwa vijana wasotea ajira walioweka kambi yao kijiji cha Soga-Kibaha, Pwani wakati akifanya mkutano nao. Mkuu huyo wa wilaya alifanya ziara hiyo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA - KAJUNASON/MMG - KIBAHA.
Sunday, October 01, 2017
WANAHABARI WATEMBELEA MITAMBO YA UZALISHA MAJI YA DAWASCO YA RUVU CHINI NA JUU
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wamefanya ziara ya siku moja katika Mitambo ya Uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini iliyopo Mlandizi na Bagamoyo mkoani Pwani ,ziara iliyoandaliwa na Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salamaa (DAWASCO) kwa lengo la kujifunza namna matibabu ya maji yanavyofanyika kuanzia yanapotoka mto Ruvu.
Mbali na kutembelea Mitambo ya uzalishaji maji pia Wanahabari hao wametembelea ofisi za Dawasco mkoa wa Tabata kujionea utendaji kazi kwa watendaji wa Shirika hilo ,kituo cha Tabata.
Meneja wa Dawasco Tabata, Victoria Masele akiwakaribisha wanahabari ofisi kwake mara baada ya kumtembelea.
Meneja Biashara wa Dawasco Tabata, Jamal Chuma kifafanua jambo kwa wanahabari.
Vifaa vilivyopo katika ofisi za Dawasco Tabata.
Mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu.
Maji yakiingia katika mitambo.
Kina cha maji kinavyoonekana.
Meneja
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Edward Mkilanya akiongea machache na wanahabari.
Mhandisi wa Mtambo wa Ruvu Chini, Emaculata Msigali akitoa ufafanuzi jinsi unavyofanya kazi.
Monday, July 10, 2017
WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA KITUO CHA AFYA CHA KATORO NA KUJIONEA HALI YA KITUO HICHO
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na
watumishi wa kitupo cha afya cha mji mdogo wa Katoro.Waziri huyo amefika
katika kituo hicho ili kujionea hali ya
kituo hicho ambacho kinahudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huo pamoja na
jirani zake licha ya kuwa na changamoto ya watumishi pamoja na miundombinu
KIWANDA CHA MCHINA CHAFUNGIWA KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb.) akiongea na baadhi ya wananchi wa
mtaa wa Mivinjeni Buguruni Sukita Alipowatembelea kufuatia kero ya
utiririshwaji wa maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali kutoka katika baadhi ya viwanda maji
yanayotumiwa na wakazi wa maeneo hayo kwa kumwagilia bustani za mboga mbonga. Kutoka
kulia kwake ni Naibu Meya wa wa Manispaa
ya Ilala Bw. Omary Kumbilamoto, Afisa Mazingira Ilala Bw. Adon Mapunda na
Diwani wa kata ya Buguruni Bw. Adam Fugane.
Friday, June 23, 2017
KUTOKA SHIMONI KABLA HUJAFA.
Watanzania wametakiwa kusimama katika zamu na nafasi zao ili
waweze kutolewa katika mashimo walikowekwa.
Kauli hiyo imetolewa na mwinjilisti wa kimataifa George
banali wakati akihubiri katika viwanja vya wapo mission International vilivyoko
mbezi Beach Jogoo jijini Dar es salaam,ambapo alisema kuwa njia pekee ya
mtanzania kufanikiwa kutoa katika shimo la mateso ni kumpa Yesu maisha yake.
Aidha alisema kuwa kutokana na watu wengi kuendelea kuteseka
na kutaabika njia moja tu ni kumpokea bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wa
maisha yako na hautaendeleea kukaa katika shimo.
Inawezekana shilo ulilowekwa ni shimo la mateso magonjwa na
shida mbalimbali pamoja na kuonewa na nguvu za giza sasa ni wakati wako wa
kufunguliwa na kuwekwa huru katika maisha yako.
Mukutano huo bado unaendelea ambapo waimbaji mbalimbali wa
nyimbo za injili wanahudumu kama vile Yes Kwaya,faraja Ntaboba,kikundi cha
kusifu na kuabudu cha BCIC na waimbaji wengine wengi.
Thursday, April 27, 2017
MIAKA 53 YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUIMARISHA, TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYWA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Kila mtanzania ametakiwa kuhakikisha anafanya jitihada za kuimarisha na kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa miaka 53 iliyopita.
Akizungumza leo wakati akihutubia wananchi katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano katika uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa ni muhimu watanzania wakalinda Muungano kwa vile una manufaa kwa nchi zote mbili.
Friday, April 21, 2017
WIZARA YA ARDHI NA MAMLAKA YA MAPATO (TRA) WAENDESHA MAFUNZO YA KODI ZA PANGO YA ARDHI NA MAJENGO KWA WAANDISHI WA HABARI
Bw. Dennis Masami Mkuu wa Kitengo cha kodi Wizara ya Ardhi akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina kuhusu Kodi za pango ya Ardhi na majengo iliyofanyika wizarani hapo ili kuwajegea uwezo wanahabari katika masuala ya sheria na taratibu za ulipaji wa kodi za pango ya Ardhi na kodi za majengo, Semina hiyo ambayo imeshirikisha pia wataalam wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) imefanyika leo jijini Dar es salaam ikishirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Wednesday, April 19, 2017
YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA TISA MKUTANO WA SSBA WA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO APRIL 19, 2017.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Bungeni leo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Mawaziri kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Aprili 19, 2017. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Monday, April 17, 2017
Friday, April 14, 2017
KUSANYIKO LA PASAKA LILILOANDALIWA NA WAPO RADIO 98.1 FM LINAENDELEA KATIKA VIWANJA VYA WAPO REDIO AMBAPO NI IJUMAA KUU NA JUMAMOSI
Mambo yanaendelea katika viwanja hivi vya wapo radio 98.1 fm
Askofu John Rwezaura akifungua Kusanyiko la Pasaka liloandaliwa na Wapo redio FM.
Askofu John Rwezaura akifungua Kusanyiko la Pasaka liloandaliwa na Wapo redio FM.
Monday, April 10, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo tarehe 9 Aprili 2017 amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean jijini DSM na kutoa wito kwa watanzania kumuunga mkono katika kusaidia watu wenye mahitaji ikiwa ni pamoja na wagonjwa.
Mama Janeth Magufuli amesema ameamua kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa hospitalini hapo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa yeye alizaliwa katika hospitali hiyo tarehe na mwezi kama wa leo
Aidha ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini magonjwa yanayoweza kutibika yakiwa katika hatua za awali.
Mama Janeth Magufuli amewapa pole wagonjwa wote waliolazwa hospitalini hapo na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Pia amewapongeza Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean road kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutibu wagonjwa hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemshukuru mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia wagonjwa hospitali hapo na kuahidi kuendelea kumuunga mkono katika jitihaa zake hizo kama walivyofanya leo.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dakta Julius Mwaisalage amemshukuru mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kwa kusaidia wagonjwa hospitalini hapo kwa kuwa kitendo hicho kinawatia moyo wao kama wauguzi lakini pia kinarudisha imani kwa wagonjwa na kujiona kuwa hawapo peke yao.
Mama Janeth Magufuli kwa kushirikiana na wanawake wa Wilaya ya Ilala na Temeke wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wametoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mchele,Maharage,sabuni za kufulia,sabuni za kuogea, maziwa ya unga,Juisi ,taulo za kike, vitenge,kanga, misuli,mafuta ya kujipaka na dawa za meno.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata ya Kivukoni na Sea View ambazo zipo jirani na hospitali hiyo.
APRIL 09,2017,DR JULIUS MWAISALAGE ...MKURUGENZ...
APRIL 09,2017, CUTS ZA WATU NA JENGO MH MKE WA ...
APRIL 09,2017,ndugu SOPHIA MJEMA..MKUU WA WIALY...
APRIL 09,2017,UU UPSOUND ZA KUOMBEA NA KUTOA MS...
APRIL 09,2017, CUTS ZA KUTOA MSAADA NA KUTEMBEL...
APRIL 09,2017, MH MKE WA RASI MAMA MAGUFULI ASH...
Friday, April 07, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)