Friday, April 21, 2017

WIZARA YA ARDHI NA MAMLAKA YA MAPATO (TRA) WAENDESHA MAFUNZO YA KODI ZA PANGO YA ARDHI NA MAJENGO KWA WAANDISHI WA HABARI

1
Bw. Dennis Masami Mkuu wa Kitengo cha kodi Wizara ya Ardhi akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina kuhusu Kodi za pango ya Ardhi na majengo iliyofanyika wizarani hapo ili kuwajegea uwezo wanahabari katika masuala ya sheria na taratibu za ulipaji wa kodi za pango ya Ardhi na kodi za majengo, Semina hiyo ambayo imeshirikisha pia wataalam wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) imefanyika leo jijini Dar es salaam ikishirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

2
Baadhi ya wataalamu mbalimbali kutoka wizara ya ardhi na waandishi wa habri wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika leo wizarani hapo kuhusu masuala ya kodi za pango ya ardhi na kodi za majengo.
3
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
4
Wanahabari wakiandika mambo muhimu yaliyotolewa katika mada zilizotolewa na wataalam mbalimbali kutoka wizara ya Ardhi na Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu Kodi ya Pango ya Ardhi na kodi ya Majengo.
5
Maya Magimba Afisa Msaidizi wa Huduma kwa mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA)akitoa mada katika semina hiyo.
67
Bw. Gabriel Mwangosi Meneja Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye semina hiyo.
8
Stoney Mkamba Afisa Kodi Mkuu Makao Makuu TRA akifafanua jambo wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo jijini Dar es salaa.

No comments:

Post a Comment