Monday, April 10, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo tarehe 9 Aprili 2017 amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean jijini DSM na kutoa wito kwa watanzania kumuunga mkono katika kusaidia watu wenye mahitaji ikiwa ni pamoja na wagonjwa.
Mama Janeth Magufuli amesema ameamua kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa hospitalini hapo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa yeye alizaliwa katika hospitali hiyo tarehe na mwezi kama wa leo
Aidha ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini magonjwa yanayoweza kutibika yakiwa katika hatua za awali.
Mama Janeth Magufuli amewapa pole wagonjwa wote waliolazwa hospitalini hapo na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Pia amewapongeza Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean road kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutibu wagonjwa hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemshukuru mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia wagonjwa hospitali hapo na kuahidi kuendelea kumuunga mkono katika jitihaa zake hizo kama walivyofanya leo.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dakta Julius Mwaisalage amemshukuru mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kwa kusaidia wagonjwa hospitalini hapo kwa kuwa kitendo hicho kinawatia moyo wao kama wauguzi lakini pia kinarudisha imani kwa wagonjwa na kujiona kuwa hawapo peke yao.
Mama Janeth Magufuli kwa kushirikiana na wanawake wa Wilaya ya Ilala na Temeke wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wametoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mchele,Maharage,sabuni za kufulia,sabuni za kuogea, maziwa ya unga,Juisi ,taulo za kike, vitenge,kanga, misuli,mafuta ya kujipaka na dawa za meno.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata ya Kivukoni na Sea View ambazo zipo jirani na hospitali hiyo.
APRIL 09,2017,DR JULIUS MWAISALAGE ...MKURUGENZ...
APRIL 09,2017, CUTS ZA WATU NA JENGO MH MKE WA ...
APRIL 09,2017,ndugu SOPHIA MJEMA..MKUU WA WIALY...
APRIL 09,2017,UU UPSOUND ZA KUOMBEA NA KUTOA MS...
APRIL 09,2017, CUTS ZA KUTOA MSAADA NA KUTEMBEL...
APRIL 09,2017, MH MKE WA RASI MAMA MAGUFULI ASH...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment