Katika picha kijana
ambaye jina lake halikupatikana akimwagilia maji yanayosadikiwa kuwa na
kemikali mbogamboga aina ya majani ya Maboga zinazochipua katika eneo la mtaa
wa mivinjeni buguruni sukila. (Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limepewa siku saba kukagua na kujiridhisha
na uzalishaji, management na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004
na kanuni zake kwa Kiwanda cha ANBANGS kinachotengeneza mifuko aina ya viroba
vinavyotumika kama vifungashio vya saruji, sukari na aina nyingine ya nafaka, na
kukifunga kwa kile kinachodaiwa kukaidi maagizo ya serikali ya awamu ya tano ya
kutokulipa faini kwa uchafuzi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya
Makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alitoa agizo hilo Leo
alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Buguruni baada ya kupata malalamiko
yaliyoibuliwa na wakazi wa mtaa wa sukita mivinjeni kupitia kituo cha ITV ambapo Naibu waziri Mpina alitembelea eneo hilo na
kujionena namna ambavyo kiwanda hicho kinavyoendelea kutiririsha maji machafu.
Akiwasilisha taarifa
ya ukaguzi wa kiwanda hicho Bw. Jafari Chimgege ambae ni Mratibu wa mazingira
kutoka NEMC kanda ya Mashariki alimueleza Naibu waziri Mpina, kuwa “Kama
unakumbuka Mhe. Waziri Tulikuja hapa mwaka jana Novemver na tukafanya ziara na
ukaguzi hapa na kila tukija hapa hawa wachina wanashindwa kuonyesha ushirikiano
na kusema kuwa wao hawajui lugha ya Kiswahili, tuliona makosa mengi na
tuliwatoza faini ya shilingi milioni 25, na ilitakiwa walipe ndani ya wiki
mbili, lakini Mhe. Hiyo Faini haikulipwa. Na bado wanaendelea na uchafuzi wa
mazingira pamoja na kukaidi agizo za serikali.” Alisisistiza Chimgege.
Pamoja na maelezo
hayo ya Bw. Chimgege Naibu Waziri alielekeza Baraza hilo kupitia documents zote muhimu zinazohusu,
kiwanda hicho ambacho awali hakikuwa na cheti ya tathmini ya athari ya
mazingira wala vibali ya aina yoyote ya kutirirsha maji yaliyotibiwa na
kuuganishwa na mfumo wa mji taka wa DAWASCO hali ambayo ilimpelekea Mpina
pamoja na hilo kuagiza wamiliki wa kiwanda hicho kufikishwa mahakamani
Katika Ziara zake
za ukaguzi wa Mazingira na viwanda
jijini Da es Salaam, Mpina amehadi kuingia hatua ya kushirikiana na mamlaka
husika kuchukua sampuli za maji yanayopita katika bonde la mto msimbazi katika
eneo la viwanda vya karibu na mtaa wa sukita mivinjeni ili kuyafanyia vipimo na
kijirisha kama yana madhara kwa viumbe hai na mazingira hususani mboga mboga
zinazomwagiliwa maji katika maeneo.
No comments:
Post a Comment