Daraja la Makutopora linalounganisha Wilaya ya Chemba na Manyoni likiwa limekamilika kujengwa, daraja hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 628,247,000 na kisha kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima. Mbijima amewaasa wananchi wa wilaya zinazounganishwa na daraja hilo kutumia fursa ya uwepo wa barabara na miundombinu mizuri katika kuboresha maendeleo yao.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akipita katika daraja la Makutopora linalounganisha Wilaya ya Chemba na Manyoni likiwa limekalika kujengwa, daraja hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 628,247,000 kutoka serikali kuu na kisha kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akizungumza na wanafunzi na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa madarasa mawili na matundu ya vyoo nane katika sekondari ya Chikuyu yenye thamani ya shilingi milioni 108, 448,49.
Afisa wa mradi akitoa maelezo ya mradi wa ufuatiliaji naudhibiti wa mbu waenezao malaria, huku gharama ya mradi huo ikiwa ni shilingi milioni sita na nusu.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa kituo cha maarifa ya kupambana na ukimwi chenye thamani ya shilingi 87,584, 007. Mbijima amewaasa wakazi wa Manyoni kukitumia kituo hicho ili kiwasaidie katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akigawa vyandarua kwa wanawake wajawazito na wenye watoto wadogo, vyandarua hivyo ni sehemu ya mradi wa ufuatiliaji naudhibiti wa mbu waenezao malaria, hukugharama ya mradi huo ikiwa ni shilingi milioni sita na nusu.
Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya Manyoni Bw.Ally Mimbi akisoma taarifa ya ujejzi wa daraja la Makutopora linalounganisha Wilaya ya Chemba na Manyoni likiwa limekalika kujengwa, daraja hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 628,247,000 kisha kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima.
No comments:
Post a Comment