Thursday, September 22, 2016

DAR, PWANI KUKOSA MAJI KWA SAA 12

SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza kuwapo kwa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam, pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kwa wastani wa saa 12 siku ya Jumamosi.

Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza sababu ya kuzimwa kwa mitambo hiyo ni kuruhusu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufanya matengenezo kwenye laini kubwa ya umeme inayotoka Ubungo kwenda kituo cha Tanesco Mlandizi, ambacho kinapeleka umeme kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini.

“Kutokana na Matengenezo hayo yatakayofanywa na Tanesco yatapelekea ukosefu wa huduma ya Maji kwa wakazi wa maeneo ya Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, na Luguruni,”

“Mji Wa Bagamoyo, Vijiji Vya Mapinga, Kerege na Mapunga. Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe” alisema Lyaro.

Maeneo mengine yaliyotajwa ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali Ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Changombe, Keko pamoja na Tabata. 

“Tunaomba wananchi wahifadhi Maji kwa kipindi hiki ili wasipate shida wakati tutakapozima mitambo hiyo”. alisema Bi.Lyaro 

No comments:

Post a Comment