Tuesday, October 25, 2016

WATU 12 WAMERIPOTIWA KUUWAWA KATIKA SHAMBULIO LILOTEKELEWA NA KUNDI LA AL-SHABAB HUKO MANDERA,KENYA.

Washambuliaji walirusha vilipuzi kwenye jumba hilo

Image copyright
Watu 12 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba moja ya malazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe amesema watu sita wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ya Bishaaro.
Wanamgambo wanaoaminika kuwa wa kundi la al-Shabaab walishambulia nyumba hiyo mwendo wa saa tisa unusu usiku. Walirusha vilipuzi kwenye nyumba hiyo kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi waliokuwemo ndani.
"Sehemu ya jumba iliporomoka, na kuua watu 12. Watu sita wametolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo wakiwa hai kufikia sasa," ameandika Bw Kiraithe kupitia mtandao wa Twitter.
Wataalamu wa mabomu wanafanya uchunguzi kubaini ni vilipuzi vya aina gani vilitumiwa kutekeleza shambulio hilo.
Mandera
Image captiKundi la al-Shabaab limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Mji wa Mandera upo mpakani mwa Kenya,Somalia na Ethiopia
Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.
Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia watu ambao si wa asili ya Kisomali.
Maafisa wa usalama nje ya hoteli ya Bishaaro
Mafisa wa usalama nje ya hoteli ya Bishaaro walinda usalama,
Source BBC
Image copyright

No comments:

Post a Comment