Monday, October 24, 2016

NDALICHAKO, MAHIGA WAWAVURUGA CHADEMA..... CCM WAJICHAGULIA MEYA BILA MPINZANI

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeususia uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, hali iliyopelekea wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya uchaguzi peke yao na kuwapigia kura wagombea wao bila upinzani.

CCM wamemchagua Benjamin Sitta kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kura zote 18 za wajumbe wa chama hicho. George Manyama amepata Baraka za wajumbe hao wa chama tawala kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

Chadema waliususia uchaguzi huo kwa madai kuwa CCM wamechakachua kwa kuwaleta Profesa Joyce Ndalichako (Waziri wa Elimu) na Balozi Agustine Mahiga (Waziri wa Mambo ya Nje) kupiga kura katika Manispaa hiyo ili hali waliapa na kusajiliwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Hivyo, sio wajumbe halali wa Kinondoni na hawakupaswa kupiga kura.

Wajumbe wa Chadema wanadai kuwa uchaguzi uliofanywa na CCM peke yao sio halali kwani pamoja na mambo mengine akidi ambayo ni 2/3 ya wajumbe waliopaswa kufanya uchaguzi huo kuwa halali haikutimia.

Chadema imepanga kupinga uchaguzi huo mahakamani.

No comments:

Post a Comment