Friday, October 21, 2016

NAMAINGO KUWANUISHA WAJASIRIAMALI 3000 KWA MRADI WA KUKU CHOTARA WA THAMANI YA SH. BIL. 30.

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Namaingo Business Agency (T) LTD, Ubwa Ibrahim akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wajasiriamali kuhusu jinsi ya kuzichangamkia fursa mbalimbali za ujasiriamali katika Makao Makuu ya kampuni hiyo, Ukonga, Dar es Salaam leo.

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Namaingo Business Agency (T) LTD, Ubwa Ibrahim akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wajasiriamali kuhusu jinsi ya kuzichangamkia fursa mbalimbali za ujasiriamali katika Makao Makuu ya Taasisi  hiyo, Ukonga, Dar es Salaam jana.
Kushoto ni Mratibu wa Wanahabari wa kampuni hiyo, Jamila Abdalah.
 Ubwa akifafanua jambo wakati wa mkutano huo, ambapo aliwaomba wananhabari kutumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi kuhusu fursa hizo za ijsiriamali ili waondokane na umasikini.

 Baadhi ya wanahabari na wajasiriamali wakaiwa katika mkutano huo

KAMPUNI ya Namaingo Business Agency (T) LTD, mwezi ujao inazindua mradi mkubwa wa ufugaji kuku chotara wenye thamani ya sh. bilioni 30 utakaowawezesha wananchi 3000 wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya kampuni hiyo, Ukonga, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ubwa Ibrahim  amesema mradi huo mkubwa na wa aina yake umeanza kujengwa Lindi Vijijini.

Amesema kuwa watakaonufaika ni wananchi wa mikoa hiyo watakao timiza taratibu zote, ambapo kila mmoja atakopeshwa na benki sh. mil. 10 ambazo zitakwenda moja kwa moja kwenye mradi wa kuku utakaokuwa unaendeshwa na watalaamu kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Anasema kuwa mradi mzima utasimamiwa na JKT kwa ushirikiano na Kampuni ya Namaingo ambapo mfugaji atafaidika kwa kupata faida baada ya mauzo yatakayokatwa gharama zote za mradi huo.

Katika mradi huo kila mwanachama atajengewa banda la kufugia kuku chotara 1000 watakaofugwa kisasa na kwa utalaamu unaotakiwa ili kupata kuku wenye ubora na kilo nyingi hivyo kuuzwa kwa bei nzuri.

Alitaja baadhi ya vigezo na taratibu anazotakiwa mwanachama kukamilisha kabla ya kupatiwa mkopo huo kuwa ni; Kwanza kuwa mwanachama wa Namaingo, kufungua akaunti katika benki za NMB, CRDB,  pia kujiunga na NSSF, NHIF, PSPF, Bima ya Maisha, kusajili jina la biashara Brela.

Pia mwanachama anatakiwa kuwa na Tin number,  ajiunge Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja (UTT-AMIS),  awe na leseni ya biashara, cheti cha TDFA, cheti cha GSI, cheti cha TBS bila kusahau kopi ya kitambulisho cha mpigakura, leseni ya udereva au kitambulisho cha utaifa.

Pia Kampuni hiyo inatarajia kufungua miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji mikoani itakayowanufaisha wananchi wengi.

No comments:

Post a Comment