Thursday, October 06, 2016

RC WA MBEYA AMOS MAKALLA ATOA TAMKO KUFUATIA TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI WA MBEYA DAY


Tukio lilianza tarehe Jumatatu 26/9/2016, ambapo Mwalimu Frank Msigwa, mwanafunzi kwa vitendo kutoka chuo kikuu cha  Dar Es  salaam ambapo alitoa assignment ya somo la kingereza kwa wanafunzi wa kidate cha tatu.

Baada ya kusahihisha, aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya. Hivyo,tarehe Jumatano 28/9/2016,alikwenda darasani na kutoa adhabu wale ambao hawajafanya kazi yake.Alianza kwa kuwapa adhabu ya push-up,kisha kupiga magoti na baadae aliwapuga viboko viwili.Katika utekelezaji wa adhabu ile, mwanafunzi  Sebastian Chingulu alikataa kufanya  kutokana na kuumwa na goti.

Baada ya kuigomea adhabu ile, Mwalimu Frank Msigwa na wenzake wawili, John Deo na Sanke Gwamaka, walimpeleka ofisini na kuanza kumshambulia kwa kipigo kama inavyoonekana kwenye video.Baada ya tukio hilo waalimu hao walitoweka shuleni hapo.Wakati wanamshambulia mwanafunzi huyo, kulikuwepo na Mwalimu mwingine aliyewasihi wasiendelee kumpiga kijana huyo na ndiye aliyerekodi tukio hilo.

Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu kadhaa pamoja na Mwalimu Mkuu kwa mahojiano pamoja na kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu hiyo.Kuhusu mwanafunzi aliyepigwa,nawahakikishia kuwa serikali itawasaka popote walipo walimu  waliofanya tukio hilo na kufikisha katika vyombo vya dola ili wapate haki yao kisheria.
Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa na matibatibu.

Hii ni taarifa ya awali, nitaendelea kutoa taarifa kwa kila hatua tunayoifikia. Ni Mimi,
 

Amos G Makalla
RC Mbeya

No comments:

Post a Comment