Tuesday, October 25, 2016

WANAHABARI WAPIGWA MSASA KUHUSU KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE, USUBI, KICHOCHO, TRAKOMA

 Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga tabia ya  kutumia Kingatiba ya magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo, Usubi Matende na Mabusha wakati wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari, Dar es Salaam leo. Kampeni ya kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi takribani mil. 4 wa Jiji la Dar es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Meneja Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Upendo Mwingira akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
 Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo



 Mtangazaji wa BBC, Halima Kassim akitafakari jambo  kuhusu semina hiyo ya wanahabari kupata uelewa kuhusu magonjwa hayo na jinsi ya kuwaelimisha wananchi kutumia Kingatiba kwa kumeza  dawa mara noja kila mwaka ili kuboresha afya

 Mtaalamu Kaitaba akionesha baadhi ya dawa za Kingatiba ya magonjwa hayo

 Ofisa Habari wa Mradi huo, Said Makora akiwataka wanahabari kuwaelimiasha wananchi juu ya magonjwa hayo na jinsi ya kupata Kingatiba kwa kuandika makala, habari, majarida na kutumia mitandao ya kijamii kwa nia ya kuyatokomeza magonjwa hayo kufikia mwaka 2020.
 Kaitaba akionesha vifaa vinavyotumika kuwapima watu ili wapewe dawa kulingana na kimo chake.
 Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Jasmin akichangia mada wakati wa semina hiyo.
 Wana habari wakipatiwa dawa za Kingatiba za magonjwa hayo

Mtangazaji wa E FM Radio akipimwa urefu ndipo apatiwe dawa 

No comments:

Post a Comment