Na Barnabas Kisengi,
IMEELEZWA
kuwa Matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na unyanyasaji wa kijinsia ni kichocheo
cha umasikini kinacholeta migongano na udhalilishaji unaopelekea kurudisha
nyuma maendeleo ya Taifa .
Hayo
yamebainishwa mapema na katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo
(CHADEMA)Wilaya ya Manyoni mkoani Singida Bw.Saimon Boniphace Mtemi alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari ofisini kwake.
Mbali na
hayo alisema ,ni wajibu wa kila mtanzania kulipigia kelele suala la matumizi
mabaya ya madaraka kwa kufanya juhudi ya kuwaelimisha wengine juu ya
uwajibikaji utakaoleta amani kwenye jamii na kuepusha migongano inayoletwa na
matumizi mabaya ya madaraka.
Alisema,baadhi
ya watu wenye dhamana wamekuwa wakiwanyanyasa wananchi pindi wanapohitaji
huduma kiasi ambacho hupelekea kudai rushwa ya ngono na wakati mwingine
kunyimwa huduma.
Pia aliseama
mapambano dhidi ya rushwa ya ngono hayana uhuru na hivyo serikali kwa ujumla
inapaswa kujipanga upya ili kuongeza ari ya mapambano dhidi ya rushwa .
Hata hivyo
alisema wahanga wa rushwa ya ngono inapotokea wamedhalilishwa huwa hawajui ni
wapi pa kukimbilia kwa kuogopa fedheha kutokana na kutokuwa na uelewa wa
kutosha na hivyo ni jukumu la watanzania waelewa kuwaelimisha.
Pamoja na
hayo katibu huyo alibainisha kuwa matumizi mabaya ya madaraka ni kichocheo cha
uvunjifu wa amani ambapo hutokea baada ya udhalilishaji na kusababisha matabaka
mawili kutopana .
Hatua hii
imekuja siku chache baada ya Tanzania kuazimisha siku ya amani duniani mkoani
Dodoma ambapo jaji wa mahakama kuu ya Taifa Sofia Wambura alikiri kuwa rushwa
ya ngono bado ipo na kwamba atakaedai au kutoa rushwa ya ngono wote
watashitakiwa.
Aidha jaji
wambura alitumia fursa hiyo kwa kusema kuwa yeyote atakaebainika kupata ajira bila kuwa na vigezo kwa
kutoa rushwa sheria itachukua mkondo wake na kuwataka wananchi wote kuwa makini
ili kuepuka suala la rushwa kwa maendeleo na kuitunza amani.
No comments:
Post a Comment