Mteule huyo amesema atapunguza kodi na kufanya mageuzi ya sekta ya huduma za afya kwa kuachana na mfumo uliowekwa na Barack Obama.
Pia amesema atabadili haraka sheria juu ya uhamiaji , Hizo ni miongoni mwa hatua tatu muhimu alizoahidi kwenye kampeni zake za Urais.Alisema yeye atafanya mambo ya kuvutia kwa ajili ya watu wa Marekani. Lakini baadhi ya ahadi alizotoa kwenye kampeni zimeondolewa kwenye tovuti yake ikiwemo tishio la kupiga marufuku Waislamu kuingia Marekani, kuachana na makubaliano ya Paris katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
naye rais wa sasa wa taifa hilo Barack Obama amesema kuwa anamuunga mkono rais mteule Donald Trump
hivi ndivyo ilivyokuwa ndani ya Ikulu ya white house Rais Barack Obama walipokutana na rais mteule Donald Trump kama inavuyoonekana katika picha
Lakini yote hayakuwa kununa tu...
Melania na Michelle pia walikutana, lakini hawakuonekana kuwa na matatizo
No comments:
Post a Comment