Wednesday, November 30, 2016

UNESCO-TANZANIA YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA KUTOKAWIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KATIKA KUTEKELEZA MPANGO MKAKATI WA WIZARA MAWAKA 2016/2017

df
 Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigueas, (kulia), akiendesah semina ya mafunzo ya siku tatu kujenga uwezo kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, makao makuu ya UNESCO, Oysterbay jijini Dares Salaam, leo Novemba 30, 2016. Kushoto ni Mwanasheria wa Wizara, Bw.Evordy Kyando.
Shirika  la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni , (UNESCO), limeendesha mafunzo ya siku tatu kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ili kuwajengea uwezo wa kutekeelza mpango mkakati wa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Mafunzo hayo yaliyoanza leo Novemba 30, 2016, na kuendeshwa na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, nchini, Bi. Zulmira Rodrigues yanafanyika kwenye ofisi za shirikahilo,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
“Tumekusanyika hapa kwa mara ya kwanza kuisaidia wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezoili kuboresha uwezo wawafanyakazi wake,wafanyakazi kutoka idara tofauti tunaohapa, wapo kutoka idara ya Habari, Utamaduni, michezo pamoja na idara za kiusaidizi kama vile fedha, sheria, ICT na kadhalika.” Alianza kwa kusema Mkuuhuyo wa UNESCO.Alisema,Mpango unaweza kusaidia kufanya tathmini na marekebisho kwa mahitaji ya wizara
au taasisi yoyote ile na kwa kuzingatia hilo, Shirika hilo limeona upoumuhimowa kuwajengea uwezowatendaji katika wizara hiyo ili kutekeleza vemampango mkakati wa wizara. “Kama huna mpango wowote ule uliouweka, utajikuta
unatumia nguvu nyingi na kuishia patupu bila mafanikio yoyote yale.” Alisema.Alisema,
wafanyakazi katika taasisi yoyote ile ni wajibu kushirikiana ili kuwa na lengomoja kufikia malengo mahsusi yaliyopangwa na Wizara au taasisi. “Kabla ya kuweka mpango wowote ni lazima kufanyike utafiti wa hali halisi ya jambo
linalotaka kushughulikiwa.” Alifafanua Bi. Zulmira.Washiriki
walianza kujifunza mambo mbalimbali ama vile, namna ya kutambua tatizo lamsingi, uwezo, udhaifu, fursa na tishio mambo yote hayo yanayojulikanakitaalamu kama (SWOT Analysis), ndiyo yatakayotoa picha halisi ya namna ya kupanga mkakati na namna ya kuutekeleza mkakati huo.
Aidhawashiriki wa warsha hiyo wamefurashiswa na mafunzo hayo kwani yatasaidia kuwajengea uwezo wa kutekeelza kikamilifu malengo ya kiofisi na binafsi.
“Mafunzo haya yatanisaidia sana katika kutekeleza malengo yaliyopangwa kwani nimejifunza
njia mbalimbali za kimkakati katika kutekeleza malengo yaliyopo.” Amesemamshiriki Lorietha Lawrence, afisa habariwizara ya Habari, Utamaduni, Sanaana Michezo.Kupitiamafunzo haya, ninahakika yatasaidia kutekelza majukumu yangu ya kila siku, na
nitakachojifunza nitashirikiana na wenzangu kwenye kitengo chetu katikakutekelezaipasavyo majukumu yetu.” Alisema Afisa mwingine wa habari, Lilian.
 Baadhi ya washiriki
Mshiriki kutoka idara ya utamaduni, Sefania Molela, akizungumza
 Mshiriki kutoka idara ya Habari akizungumza
 Bi. Zumlira Rodrigues, (kulia), akiteta jambo na Afisa Mpango wa Utamaduni wa UNESCO, Rahma Sudi
 Afisa Mpango wa UNESCO, Michaela Konopikova
 Mtaalamu wa masuala ya ICT wa UNESCO, Leonard Kisenha, (katikati), na Afisa Mpango, Utamaduni wa Shirika hilo, Michaela, (kushoto0, wakitazama kitu kwenye kompyuta
 Mkufunzi wa UNESCO, Deirdre Prins-Solan
 Mshiriki kutoka idara ya utamaduni, akizungumza

 Mshiriki kutoka idara ya Michezo akizungumza
 Bi.Zulmira akiendesha mafunzo
 Maafisa mpango-Utamaduni wa UNESCO, Rehema (kulia) na Michaela wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo
 Bi.Zulmira akiendesha mafunzo
Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Evordy Kyando, akizungumza jambo

No comments:

Post a Comment