Monday, November 21, 2016

OBAMA AMESEMA SITANYAMAZA WAKATI WA UTAWALA WA TRUMP.

Bw Obama na Bw Trump walikutana White House siku mbili baada ya uchaguzi Nov. 10, 2016.

Image copyright
Image captionBw Obama na Bw Trump walikutana White House siku mbili baada ya uchaguzi
Rais wa Marekani anayeondoka Barack Obama amesema huenda akazungumza, kinyume na utamaduni wa siasa Marekani, iwapo mrithi wake Donald Trump atatishia "maadili muhimu" ya Marekani.

Huwa desturi kwamba marais wa zamani wa Marekani huwa hawajiingizi sana katika siasa baada ya kuondoka madarakani na huwa hawazungumzi kuhusu warithi wao.
Akiongea katika kikao na wanahabari wakati wa mkutano wa nchi za Asia na Pasifiki (Apec) mjini Lima, Peru, Bw Obama amesema anakusudia kumsaidia Bw Obama na kumpa muda wa kueleza maono yake.
Lakini amesema kwamba, kama raia, huenda akalazimika kuzungumza kuhusu baadhi ya mambo.
"Ninataka kuiheshimu afisi na kumpa rais mteule fursa ya kueleza msimamo wake na mipango yake bila mtu kujitokeza kumkosoa," Bw Obama alisema.
Lakini akaongeza, kwamba iwapo suala "litagusa maadili muhimu ya Marekani na imani yetu, na nafikiri kwamba inahitajika au itafaa kwangu kutetea maadili hayo, badi nitalitathmini wakati huo".
Kisha, amejieleza kama "raia wa Marekani anayejali sana taifa".
Mkutano wa Lima, Peru Novemba 20, 2016.Image copyrightREUTERS
Image captionBw Obama amehutubu katika kikao na wanahabari mkutano wa Apec mjini Lima, Peru
Akiongea katika kikao cha wanahabari wakati wa kufungwa kwa mkutano mkuu wa viongozi wa Apec, Bw Obama amesisitiza kwamba ataonyesha utaalamu kwa kundi la Bw Trump wakati wa mpito sawa na ilivyofanyika kwa kundi lake wakati wa kuondoka kwa mtangulizi wake George W Bush.
Bw Bush, tangu aondoke madarakani, amejizuia kuzungumzia utawala wa Bw Obama. "Sidhani hilo linasaidia kwa vyovyote," aliambia CNN mwaka 2013, baada ya Obama kuchaguliwa kwa mara ya pili.
"Ni kazi ngumu. Ana mambo mengi ya kushughulikia kwenye ajenda yake. Rais wa zamani hafai kuyafanya mambo kuwa magumu zaidi kwake. Marais wengine wa zamani wamechukua uamuzi tofauti; huu ni wangu."


Msimamo wa Bw Bush unafuata desturi, ambapo maras wa Marekani huwa wanajiepusha kuwakosoa watangulizi au warithi wao.
Bw Obama alisema wazi kwamba hataingilia msimamo wa Bw Trump kabla ya muhula wake kumalizika Januari mwakani.
Lakini ufafanuzi wake kwamba, atakapokuwa raia wa kawaida, atatettea "maadili muhimu", ameutoa huku kukiendelea kuwa na wasiwasi miongoni mwa makundi ya kutetea haki za kiraia kuhusu watu wanaoteuliwa na Bw Trump kushikilia nyadhifa kuu katika serikali yake.
Mwanamikakati mkuu wa Bw Trump, Steve Bannon, alikuwa awali mkuu wa Breitbart, tovuti ambayo imetuhumiwa kwa kuendeleza ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Wayahudi. Na mshauri mkuu wa masuala ya usalama wa taifa wa Bw Trump, Jenerali Michael Flynn, alikuwa awali amefananisha Uislamu na "saratani" ambayo inaenea Marekani.
Barack Obama.Image copyrightAFP
Mwanasheria mkuu aliyeteuliwa na Bw Trump, Jess Sessions, alizuiwa kuhudumu kama jaji wa dola mwaka 1986 kwa sababu ya kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi.
Bw Obama amesema anaamini majukumu makuu ya urais yatamlazimu Bw Trump kulegeza baadhi ya sera zake kali ambazo alizitetea wakati wa kampeni.
Alipoulizwa kuhusu kushindwa kwa chama cha Democratic chini ya Hillary Clinton, Bw Obama alikosoa kampeni zilizolenga "makundi fulani", badala ya kukumbatia taifa lote.
Bi Clinton amekosolewa kwa kuangazia sana watu wa jamii fulani, wakiwemo Walatino na wanawake, ambao waliaminika kumuunga mkono badala ya watu wote.
Njia kama hiyo "haitakusaidia kushinda uungwaji mkono wa watu wengi kama inavyohitajika," Bw Obama alisema na kuongeza kwamba chama hicho kilihitaji "ujumbe bora zaidi".

No comments:

Post a Comment