RAIS WA 45 WA MAREKANI DONALD TRUMP AWEKA WAZI VIPAUMBELE VYA SERA ZAKE
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
Image copyright Baada ya mkutano na msemaji wa Republican Paulo Ryan, rais mteule wa Marekani Bwana Donald Trump ameeleza vipaumbele vya sera zake.
Mteule huyo amesema atapunguza kodi na kufanya mageuzi ya sekta ya huduma za afya kwa kuachana na mfumo uliowekwa na Barack Obama.
Pia amesema atabadili haraka sheria juu ya uhamiaji , Hizo ni miongoni mwa hatua tatu muhimu alizoahidi kwenye kampeni zake za Urais.Alisema yeye atafanya mambo ya kuvutia kwa ajili ya watu wa Marekani. Lakini baadhi ya ahadi alizotoa kwenye kampeni zimeondolewa kwenye tovuti yake ikiwemo tishio la kupiga marufuku Waislamu kuingia Marekani, kuachana na makubaliano ya Paris katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
hivi ndivyo ilivyokuwa ndani ya Ikulu ya white house Rais Barack Obama walipokutana na rais mteule Donald Trump kama inavuyoonekana katika picha
Image copyrightREUTERSImage captionNikiangalia sana pale mbali, haya masaibu yote yatapita...Image copyrightREUTERSImage captionFikira za Trump zinaonekana kuyumba ... labda kwa kukumbuka aibu iliyotokana na utani kuhusu kuzaliwa kwa Obama mwaka 2011.Image copyrightEUROPEAN PHOTOPRESS AGENCYImage captionWanasalimiana lakini macho yako wapi.... taama mdomo wa TrumpImage copyrightAFPImage captionTena, sasa Obama anamwangalia Trump.... lakini Trump anaamua, la hasha, SIWEZI kumwangalia machoniImage copyrightREUTERSImage captionKupeana mikono kwisha sasa, na ni furaha sana kwa Trump .... lakini anaonekana kutoyaamini anayoyasema Rais Obama
Lakini yote hayakuwa kununa tu...
Image copyrightEUROPEAN PHOTOPRESS AGENCYImage captionWawili hao walicheka wakati mmoja walipotaniana.
Melania na Michelle pia walikutana, lakini hawakuonekana kuwa na matatizo
Image copyrightWHITE HOUSEImage captionMelania Trump na Michelle Obama wakiwa ikulu ya White House
Kampeni za Trump zisingeweza kusema kuhusu mabadiliko hayo ya tovuti.
No comments:
Post a Comment